Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Mauritius wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua mkutano huo mjini Port Louis Machi 23, 2017. ......................................................
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali chini ya Mheshimiwa Rais
Dkt. John Magufuli inautashi wa dhati wa kuboresha mazingira ya uwekezani na
biashara nchini kwa kuondoa rushwa na urasimu katika sekta ya umma, hivyo
amewakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara wa Mauritius kuja nchini.
Amesema
Tanzania imefanya mageuzi makubwa ya kiuchumi kwa kubadili mifumo yake ya
kisheria, kitaasisi na kifedha ili kuhakikisha wawekezaji wanahudumiwa ipasavyo
na kupewa umuhimu wanaostahili kwani ni wadau muhimu kwa maendeleo ya Taifa.
Waziri
Mkuu amesema hayo jana wakati akifungua kongamano la Biashara na
Uwekezaji kati ya Tanzania na Mauritius lilifanyika katika Hotel ya Labourdonnaise mjini Port
Louis nchini Mauritius.
Kongamano hilo liliandaliwa na Kituo cha
Uwekezaji Tanzania (TIC).
“Kwa niaba
ya Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli nawakaribisha kwa mikono miwili kuja na kuwekeza nchini katika sekta mbalimbali
zikiwemo za viwanda na utalii na kutembelea vivutio vya utalii na kupata burudani
ya aina yake na kwa wafanyabiashara Tanzania ni mahali pazuri kwa kuwekeza,”
alisema.
Kongamano hilo lilihudhuriwa na Waziri Mkuu wa Mauritius
Mheshimiwa Pravind Kumar Jugnauth, Prime Minister of the Republic of
Mauritius; Waziri wa Mambo ya Nje wa Mauritius.
Wengine ni
Mwenyekiti wa Taasisi
ya Sekta Binafsi (TPSF), Godfrey Simbeye,, Executive
Director of Tanzania Investiment Centre; Mkurugenzi
Mtendaji wa
TIC Bw. Clifford Tandar pamoja na Maofisa wa Serikali ya Tanzania na Mauritus.
|
Post a Comment