BOT - " Mfumuko wa Bei Utokanao na Ongezeko la Fedha ni Hatari Katika Uchumi wa Nchi "
Mchumi Mwandamizi wa Benki Kuu ya Tanzania,
(BoT), kutoka Kurugenzi ya Utafiti na Sera za Uchumi, Bw. Lusajo Mwankemwa, akiwasilisha mada juu ya Sera ya Fedha ya Benki Kuu ya Tanzania, wakati wa semina ya Wiki moja kwa waandishi wa habari za Uchumi na Fedha kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, tawi la Zanzibar, leo Machi 28, 2017.
...............................................
Na Khalfan Said
Na Khalfan Said
Mfumuko wa bei Utokanao na ongezeko la Fedha ni hatari sana katika uchumi wa nchi,
Mchumi Mwandamizi wa Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), kutoka Kurugenzi ya Utafiti
na Sera za Uchumi, Bw. Lusajo Mwankemwa,
ameiambia semina ya Waandishi wa habari za Uchumi na Fedha kutoka vyombo
mbalimbali vya habari leo Machi 28, 2017.
Semina
hiyo ya wiki moja inayoendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya
Tanzania tawi la Zanzibar, ina lengo la kuwaelimisha waandishi wa habari kuhusu
namna bora ya uandishi w ahabari za uchumi na fedha.
Chini
ya Sera ya Fedha, (Monetary Policy), Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), kama
mtengeneza fedha (mchapishaji), inaweza kudhibiti mfumuko wa bei utokanao na
ujazi wa fedha kutokana na viashiria vya uwezo wa uzalishaji katika taifa
unapopungua au kuonegzeka.
Sera ya fedha maana yake ni pale Benki Kuu inapoamua kuongeza fedha kwenye mzunguko au kupunguza na hii itategemea sana na uzalishaji bidhaa, alifafanua Lusajo.
Sera ya fedha maana yake ni pale Benki Kuu inapoamua kuongeza fedha kwenye mzunguko au kupunguza na hii itategemea sana na uzalishaji bidhaa, alifafanua Lusajo.
Meneja Uhusiano wa Umma na Itifaki wa Benki Kuu ya Tanzania, BoT), Bi. Zalia Mbeo, akifafanua baadhi ya hoja zilizoulizwa na waandishi wa habari kuhusu mada ya Sera ya Fedha.
Baadhi wa Waandishi wa habari wakifuatilia mada hiyo.
Meneja Msaidizi-Idara ya Uhusiano wa Umma, Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), Bi. Vicky Msina akizunhuzma mwanzoni mwa warsha hiyo.
Mwandishi wa habari za Biashara na Uchumi wa Azam TV, Bi. Rahma Salum akizungumza.
Post a Comment