Naibu Waziri MASAUNI awaagiza Maafisa Magereza Kuongeza Kasi ya Uzalishaji
Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa suti) akiongozwa na Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, (CGP) Dkt. Juma Malewa (mbele), kuingia ukumbini
kwa ajili ya kufungua Mkutano wa Maafisa Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi
la Magereza pamoja na Wakuu wa Vituo vya Magereza Tanzania Bara, uliofanyika
Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam leo.
..................................
..................................
Suleiman Msuya
Masuani alisema hayo wakati akizungumza katika mkutano wa wakuu wa vituo vya magereza Tanzania Bara uliofanyika katika Bwalo la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri alisema iwapo wakuu wa magereza watatumia wafungwa waliopo uzalishaji utaongezeka hivyo kuondokana na tabia ya kulalamika ufinyu wa bajeti.
Alisema pamoja na vigezo mbalimbali vya kupima wakuu wa magereza kigezo kingine kitakuwa ni kuangalia kasi ya uzalishaji kwa eneo husika.
Masauni alisema jeshi la magereza lina rasilimali nyingi kama mashamba na viwanda hivyo wanapaswa kutumia fursa iliyopo kuongeza uzalishaji na kuchochea uchumi wa viwanda.
“Napenda kuwa muwazi hatutavumilia mkuu yeyote wa gereza ambaye atashindwa kuzalisha na kuendeleza fursa ambazo zinamzunguka kwani Tanzania ya viwanda itafanikiwa kupitia vyombo vilivyopo katika wizara yetu,” alisema.
Alisema katika kutatua changamoto ta usafiri wanatarajia kupokea magari 450 siku za karibuni katiya 905 ambayo wameahidiwa na Serikali hali ambayo itaweza kutatua changamoto hiyo.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Maafisa
Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza naWakuu wa Vituo vya
Magereza yote Tanzania Bara (hawapo pichani) katika Mkutano uliofanyika katika
Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi
hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam leo.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, (CGP) Dkt. Juma Malewa akitoa hotuba yake
ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni (kulia) kwa ajili ya kuja kuufungua Mkutano wa Wakuu wa Vituo vya
Magereza Tanzania Bara ambao pia ulihudhuriwa na Maafisa Waandamizi wa Jeshi
hilo kutoka Makao Makuu, ulifanyika Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga,
jijini Dar es Salaam leo.
Hata hivyo, Dkt Malewa katika hotuba yake alimshukuru Rais John Magufuli kwa kutatua kwa kiasi kikubwa changamoto ya uhaba wa nyumba za Makazi ya Askari wa Jeshi hilo pamoja na juhudi za Serikali yake za ununuzi wa magari 450 kwa awamu ya kwanza ambapo jeshi hilo linatarajia kuyapata. Katikati ni Naibu Kamishna wa Jeshi hilo, Edith Mallya.
Hata hivyo, Dkt Malewa katika hotuba yake alimshukuru Rais John Magufuli kwa kutatua kwa kiasi kikubwa changamoto ya uhaba wa nyumba za Makazi ya Askari wa Jeshi hilo pamoja na juhudi za Serikali yake za ununuzi wa magari 450 kwa awamu ya kwanza ambapo jeshi hilo linatarajia kuyapata. Katikati ni Naibu Kamishna wa Jeshi hilo, Edith Mallya.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Maafisa
Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza naWakuu wa Vituo vya
Magereza yote Tanzania Bara katika Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga,
jijini Dar es Salaam leo.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia
waliokaa), Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, (CGP) Dkt. Juma
Malewa (wapili kushoto waliokaa), Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi hilo, Gaston
Sanga (kulia waliokaa), Naibu Kamishna wa Jeshi hilo, Edith Mallya (kushoto)
wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Jeshi hilo, mara baada ya Naibu
Waziri huyo, kuufungua Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Makao Makuu ya Jeshi
hilo pamoja na Wakuu wa Vituo vya Magereza Tanzania Bara, uliofanyika Bwalo Kuu
la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam.
Post a Comment