Serikali yaunda Kamati Kuchunguza Mkasa Uliotokea CLOUDS MEDIA GROUP
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ameunda kamati ya
watu watano kuchunguza suala la kilichotokea Clouds Media siku ya Alhamisi
pamoja na Ijumaa usiku.
Kamati
hiyo imeundwa baada ya Waziri Nape kufanya ziara Clouds Media leo Jumatatu
20/03/2017 na kuzungumza na uongozi wa Clouds Media kufuatia tukio la Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam kutembelea ofisi hizo siku ya Ijumaa usiku akiwa na
askari wenye silaha.
Kamati
hiyo itaongozwa na Mwenyekiti Dkt. Hassan Abbas Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO,
Bw. Deodatusi Balile Makamu Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri, Ndg. Jesse
Kwayu Mhariri Mtendaji Gazeti la Nipashe, Ndg. Mengida Johannes kutoka Wapo
Redio pamoja Ndg. Mabel Masasi kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Baada
ya kamati hii kufanya uchunguzi wa kina na kujiridhisha kutoka pande zote mbili
Wizara itasema hatua itakazochukua.
Imetolewa na:
Zawadi Msalla
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini
Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo.
20/03/2017
Post a Comment