Mwanasoka Djibril Cisse atangaza kustaafu Soka
Mshambulizi wa zamani wa Liverpool na Ufaransa Djibril Cisse, amestaafu kutoka kwa soka akiwa na umri wa miaka 35.
Awali Cisse alisitisha taaluma yake ya kusakata dimba mwezi Oktoba 2015 kutokana na jeraha la nyonga, lakini alitumaini kurejea baada ya upasuaji.
Aliendelea kufanya mazoezi na klabu yake ya Auxerre katika harakati ya kujiimarisha, lakini baada ya kushindwa kusajiliwa, aliamua kuhitimisha taaluma yake ya miaka 17.
Cisse, sasa anaangizia taaluma yake mpya "kama produza DJ, na mchambuzi."
"Nimependa mno kuwa mwanasoka," anasema. "hadi kufikia sasa, mpira umekuwa ndio maisha yangu.
"Ningependa saana kuendelea na taaluma yangu, lakini inafaa nikiri hapa leo kuwa kandanda imemalizika."
Cisse, aliyeshinda jumla ya vikombe 41 kimataifa, aliichezea Liverpool kwa miaka mitatu tangu mwaka 2004, kabla ya kurejea katika timu yake ya nyumbani huko Ufaransa - Marseille.
Pia aliwahi kusakatia soka timu za Sunderland, Panathinaikos, Lazio, QPR, Kuban Krasnodar na Bastia.
Post a Comment