Waziri JAFO aagiza Utunzwaji wa Miundombinu ya Shule ya Chang'ombe Manispaa ya Dodoma
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Seleman Jafo akitoa agizo kwa
halmashauri, kamati za shule na mikoa nchini kuacha kufanya kazi kwa mazoea na
badala yake kutumia juhudi na maarifa ili kuwaletea wananchi maendeleo kwa
haraka. Ameridhishwa na ubora na kasi waliyoitumia kujenga majengo hayo.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Seleman Jafo akifungua mlango ili
kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa ambao umekamilika kwa asilimia mia moja.
Mojawapo
ya madarasa yaliyokamilika katika shule ya msingi Chang’ombe A Manispaa ya
Dodoma. Jumla ya vyumba vya madarasa sita vimejengwa ili kukabiliana na
changamoto ya vyumba vya madarasa katika shule hiyo inayotokana na wingi wa
wanafunzi, shule hiyo ina zaidi ya wanafunzi 2000.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Seleman Jafo akizungumza na walimu,
wanafunzi na Kamati ya shule ya msingi Chang’ombe A Manispaa ya Dodoma
alipofanya ziara kujionea maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ambao
umekamilka kwa asilimia mia moja, Kulia kwake ni Kaimu Afisa Elimu Mkoa Dodoma Tumsifu Mwasamale na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Nelly kinyaga kushoto
kwake ni Diwani Kata ya Chang’ombe Mhe.Bakari Samweli Fundikira.
...............................................
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi
ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za
Mitaa(TAMISEMI) Seleman Jafo amewataka wanafunzi na walimu wa shule ya msingi
ya Chang’ombe kutunza na kuitumia
miundombinu iliyojengwa ili kuongeza ufaulu katika shule hiyo.
Jafo ametoa kauli hiyo leo
alipotembelea shule hiyo ili kukagua utekelezaji wa agizo alilolitoa juu ya kukamilisha ukarabati wa
miundombinu katika shule hiyo ifikapo 10 januari, mwaka huu.
Novemba 3, mwaka jana Jafo
alitoa agizo kwa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kuhakikisha inakamilisha
ujenzi wa matundu 20 ya vyoo na vyumba vya
madarasa 8 pamoja na ukarabati wa
vyumba vya madarasa 2 katika shule ya
Chan’gombe A ifikapo januari, 10 mwaka
huu kabla ya msimu wa masomo kuanza.
Katika ziara
hiyo, Jafo amesema ameridhishwa kwa hatua nzuri
ya ukarabati huo na kupongeza uongozi wa Halmashauri ya Manispaa , kamati ya shule ya Chang’ombe
,walimu na Diwani wa Kata ya Chang’ombe kwa utekelezaji huo.
Amesema shule hiyo
inapaswa kuongeza ufaulu wake ili iwe mfano mzuri wa kuigwa kwa shule nyingine
.
Amebainisha awali alitoa agizo
hilo baada ya kubaini changamoto mbalimbali katika shule ya msingi ya
Chang’ombe A .
‘’Maagizo niliyoyatoa yalikuwa magumu sana
lakini nia yangu ilikuwa kuwatengenezea mazingira rafiki wanafunzi na walimu , nimefarijika na utekelezaji wake, hali
haikua nzuri hapo mwanzo lakini nimefarijika kwa kazi nzuri, muonekano wa madarasa
unaridhisha nawapongeza sana’’ amesema Naibu Waziri huyo
Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Nelly Kinyaga
ameishukuru serikali kwa kuboresha miundombinu ya shule hiyo ambapo awali mazingira ya shule hiyo yalikuwa
sio rafiki kwa wanafunzi na walimu kutokana na
upungufu wa matundu 20 ya vyoo na
vyumba vya madarasa 8.
‘’Kwakweli kulikuwa na
changamoto sana wanafunzi walikua wengi na madarasa machache lakini kwasasa hatuna watoto wanaokaa chini
na msongamano wa wanafunzi darasani umepungua kwa kiasi kikubwa ,naishukuru serikali na Jafo kwa kutilia
mkazo ukarabati wa miundombinu ya shule
yetu’’ amesema
Mmoja wa wanafunzi wa
shule hiyo, Ally Mohamed Swalehe ameishukuru serikali kwa kuboresha miundombinu
ya shule hiyo rafiki kwa kuwa itaongeza
ufaulu katika mitihani na kuepusha
magonjwa ya milipuko shuleni hapo.
Post a Comment