Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akifuatilia maelezo ya ramani ya Makazi Mapya
ya Mhe. Waziri Mkuu Majaliwa Kassim kutoka kwa Wataalam wa maswala ya Ujenzi
kulia kwake ni Mhandisi Joseph Muhamba na wa kwanza kushoto ni Bw. Keffa Chana
wakati wa Ziara yake katika makazi hayo Septemba 2, 2016 Mlimwa Dodoma.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu)
Mhe. Jenista Mhagama (mb) amesisitiza kuwa dhamira ya Serikali kuhamia Dodoma
ipo palepale ndani ya kipindi cha miaka minne hatua kwa hatua.
Akizungumza
na waandishi wa habari Septemba 2, 2016 wakati wa ziara yake eneo la Makazi
Mapya ya Mhe. Waziri Mkuu Majaliwa Kassim yaliyopo Mlimwa Dodoma, Waziri
Mhagama alisema “Watanzania wawe na amani, dhamira yetu iko vizuri na kama Mhe.
Rais alivyosema na tunawahakikishia kwamba ndani ya kipindi hicho sisi
tumeshajipanga kuhamamia mkoani Dodoma hatua kwa hatua”.
Waziri
Mhagama alieleza kuwa shughuli za maendeleo hazitosimama kwa kuzingatia mipango
iliyopo na bajeti ya Serikali, “Niwatoe wasiwasi kwamba mipango yote ya
maendeleo haitosimama na shughuli zote za maendeleo hazitozuiwa na ujio wa
Serikali mkoani Dodoma zitafanyika kama zilivyopangwa na tutaendelea kuyafanya
hayo kwa kuzingatia Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015 Ibara ya 151 tumesema
tunahamia Dodoma na tutafanya hivyo”.Alisisitiza Mhagama
|
Post a Comment