Jeshi la Polisi Mkoani MWANZA lashiriki Maonesho ya Biashara Afrika Mashariki
Taasisi mbalimbali zikiwemo za Serikali na binafsi kutoka ndani na nje ya nchi zimeshiriki Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki, yanayofanyika viwanja vya Rock City Mall Jijini Mwanza. Maonesho hayo huandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo nchini, TCCIA.
Taasisi mbalimbali za Wajasiriamali, Wafanyabiashara na Viwanda hutumia Maonesho hayo kukutana na wateja wapya, kutangaza na hata kuuza bidhaa zake. Mbali na hilo taasisi mbalimbali hutumia fursa hiyo kukutana na wananchi na kufikisha elimu husika.
Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kwa kujumuisha vitengo vyake ikiwemo Kikosi cha Usalama barabarani na dawati la jinsia, limetumia maonesho hayo kufikisha elimu mbalimbali kwa wananchi na hata kupokea maoni kutoka kwa wananchi.
Banda la Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Kitengo cha dawati la jinsia.
Banda la Jeshi la polisi mkoani Mwanza, kitengo cha Usalama barabarani.
Maonesho hayo yalianza Agosti 26,2016 na ufungi rasmi kufanyika Agosti 30,2016 ambapo Mkuu wa Wilaya ya Ilemela alifungua Maonesho hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kama picha inavyoonekana mgeni rasmi akiwa kwenye banda la jeshi la polisi mkoani Mwanza.
Endelea kutazama picha, Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, akikagua mabanda ya washiriki mbalimbali.
Post a Comment