Baadhi ya wahandisi
wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin
Ngonyani (hayupo pichani), katika mkutano wa 14 wa Siku ya Wahandisi
uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia Siku ya Wahandisi
Eng. Ngonyani amewataka wahandisi hao kutumia fursa kuonesha uwezo wao wa
kupanga na kutekeleza miradi ya maendeleo ili kuanzisha viwanda na kufikia
uchumi wa kati ifikapo 2025.
“Mkumbuke kutekeleza
aliyoagiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kwa
kujihusisha katika utekelezaji wa miradi mikubwa nchini ikiwemo miradi ya gesi,
bomba la mafuta na ujenzi na upanuzi wa viwanja vya ndege”, amefafanua Eng.
Ngonyani.
Naye Mwenyekiti wa
Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania (ERB), Eng. Prof. Ninatubu Lema
amemhakikishia Naibu Waziri huyo kuwa watatekeleza maelekezo yote yaliyotolewa
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuja na mpango mkakati wa
utekelezaji wake.
Zaidi ya Wahandisi
2500 wameshiriki katika maadhimisho ya 14 ya Siku ya wahandisi na kujadiliana
kwa kina namna bora ya utekelezaji wa kauli mbiu ya mwaka huu isemayo ‘Tanzania kuelekea kuwa nchi ya uchumi wa
kati na kuwa nchi ya viwanda: Nini jukumu la wahandisi’.
|
Post a Comment