|
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt.
Albina Chuwa akipewa maelezo na Mhandisi wa kampuni ya Norplan Tanzania, Magesa
Juma ambaye anapima sampuli ya udogo wa eneo litakapojengwa jengo la ofisi
hiyo linalopakana na Ukumbi wa Dodoma
Convension Center unaomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Jengo hilo
litakuwa na ghorofa 6 na linatarajiwa kukamilika mwaka 2017/18.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imeitikia wito wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wa kuhamia
Dodoma kwa kuanza kujenga jengo lake mkoani humo.
Jengo hilo litakalokuwa nyuma ya Ukumbi wa Dodoma
Convension Center unaomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) litakuwa na ghorofa
6 na linatarajiwa kukamilika mwaka 2017/18.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya
kupokea taarifa ya maandalizi ya ujenzi wa jengo hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi
ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa amesema jengo la NBS lilipangwa kujengwa
jijini Dar es Salaam lakini kutokana na agizo la Rais imebidi jengo hilo lijengwe
mkoani Dodoma.
“Kabla ya agizo la Mhe. Rais, jengo la NBS lilipangwa
kujengwa Dar es Salaam na tayari maandalizi yalikuwa yameshafanyika lakini
kutokana na agizo hilo imetupasa kujenga jengo letu hapa mkoani Dodoma,”
amesema Dkt. Chuwa.
|
|
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt.
Albina Chuwa akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea eneo
litakapojengwa jengo la ofisi hiyo
linalopakana na Ukumbi wa Dodoma Convension Center unaomilikiwa na Chama
Cha Mapinduzi (CCM). Jengo hilo litakuwa na ghorofa 6 na linatarajiwa
kukamilika mwaka 2017/18.
|
|
Wahandisi wa Kampuni ya Norplan Tanzania wakiendelea
na kazi ya upimaji wa udongo kwa ajili ya upembuzi yakinifu kabla ya kuanza kwa
ujenzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu katika eneo itakapojengwa ofisi
hiyo inayopakana na Ukumbi wa Dodoma Convension Center unaomilikiwa na Chama
Cha Mapinduzi (CCM). Jengo la ofisi hiyo itakuwa na ghorofa 6 na inatarajiwa
kukamilika mwaka 2017/18. |
Kwa upande wake Mhandisi wa kampuni ya Norplan
Tanzania, Magesa Juma ambaye anapima sampuli ya udogo wa eneo litakapojengwa
jengo hilo amesema atahakikisha anafanya kazi hiyo ndani ya muda uliopangwa.
“Nimepewa siku 12 za kumaliza suala zima la upimaji wa
udongo katika eneo hili na mpaka sasa hali ni nzuri na nina uhakika kuwa
kampuni yangu itamaliza kazi hii ndani ya muda uliopangwa,” amesema Mhandisi
huyo.
Ujenzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu utaanza
rasmi mwezi Novemba 30 mwaka huu na linatarajiwa kukamilika mwaka 2017/18.
Post a Comment