Serikali yasitisha kwa Muda Utoaji Ruzuku Kwa wachimbaji Wadogo wa Madini ili Kupisha Tathmini
TAARIFA KWA UMMA
Tarehe
20 Julai, 2016, Wizara ya Nishati na Madini ilitoa Tangazo kwa Umma kuhusu
Kukaribisha Maombi ya Ruzuku Awamu ya Tatu kwa Wachimbaji Wadogo wa Madini
nchini.
Fomu
za maombi ya ruzuku hiyo zilitolewa katika Ofisi za Madini za Kanda (ZMO) na
Mikoa (RMO) zikiambatana na vipeperushi maalum vinavyoeleza mambo yote
yanayohusu ruzuku. Fomu hizo zilianza kutolewa tarehe 20 Julai, 2016 na ukomo
wake ulikuwa tarehe 9 Agosti, 2016, saa 9:30 Alasiri.
Wizara inatoa taarifa
kuwa, imesitisha
kwa muda utoaji wa Ruzuku Awamu ya Tatu ambao ulikuwa umepangwa kufanyika
tarehe 19 Septemba, 2016, hadi pale Tathmini ya fedha ya Ruzuku Awamu ya Kwanza
na ya Pili itakapofanyika.
Aidha,
tathmini hiyo itafanyika sambamba na uhakiki wa shughuli za Wachimbaji Wadogo
walioomba Ruzuku ya Awamu ya Tatu, lengo likiwa ni kujiridhisha kama Ruzuku
hizo zimetumiwa na walengwa kwa malengo yaliyokusudiwa.
Imetolewa na;
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
Tarehe 16 Septemba, 2016
Post a Comment