Kamati ya Maafa Mkoa wa Kagera Imeendelea Kupokea Misaada ya Wahisani
Serikali ya Mkoa wa Kagera leo
Septemba tayari imepokea misaada mbalimabli ya fedha taslimu na
mahitaji mbalimbali kama Sukari, Mchele, Unga, Maji ya kunywa, Sabuni,
Blanketi, Shuka Maharage, matrubali, Mbao na Sementi vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni
32.
Aidha, Kamati ya Maafa ya Mkoa
tayari imeanza kugawa mahitaji hayo kwa wananchi waliopatwa na janga la
tetemeko na kwa sasa hawana mahala pa kuishi. Baadhi ya Wananchi wa Mtaa wa
Kashabo Manispaa ya Bukoba wamegawiwa mahita ji hayo na aliyeongo zoezi hilo ni
Mkuu wa mkoa wa Kagera Mhe, Meja Jenerali Mstaafu Salim M. Kijuu ambaye ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ya mkoa.
Katika hatua nyingine Kamati ya
Maafa ua Mkoa imeamua kutoa bati 20 na sementi mifuko 5 kwa kila mwananchi
ambaye nyumba yake ilianguka kabisa au haifai kuishi tena. Aidha, wapangaji waliokuwa wanapanga katika
nyumba hizo watalipiwa kodi ya miezi sita na Serikali kila mwezi 20,000/=
Katika hatua nyingine Mkuu wa
Mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu ameandaa kikao cha harambee ya kuchangia maafa mkoani
Kagera tarehe 16.09.2016 siku ya Ijumaa katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa kuanzia saa 3:00 Asubuhi na anawaalika
wadau wote kuja kuchangia katika harambee hiyo.
Aidha kwa wale wanaotaka
kuchangia lakini hawatahudhuria wanaweza kuchangia kupitia Akaunti ya Benki
iliyopo CRDB inayojulikana kama “KAMATI YA MAAFA KAGERA CRDB BUKOBA” Akaunti
Namba. 0152225617300. Tunawashukuru wote wanaoendelea kuchangia na Mungu
awazidishie.
Imetolewa na: Sylvester M. Raphael
Afisa Habari
(Mkoa )
KAGERA
Post a Comment