Alichokizungumza Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA katika Ziara yake ya LINDI na MTWARA
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wazee wa Ruangwa ambao
walimshukuru kwa jitihada kubwa anazofanya za kuboresha maisha ya
Wanachi wa jimbo lake la uchaguzi. Alikuwa katika ziara ya jimbo lake
la uchaguzi Julai 16, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wazee wa Ruangwa ambao walimshukuru kwa jitihada kubwa anazofanya za kuboresha maisha ya Wanachi wa jimbo lake la uchaguzi. Alikuwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi Julai 16, 2016.
Alisema Serikali iliamua kuzifuta
tozo hizo baada ya kubainika kuwa zilikuwa zikiwanyonya wakulima hali
iliyosababisha wauchukie mfumo wa stakabadhi ghalani.
“Kuanzia mwaka huu Serikali
imeamua mfanyabiashara yeyote wa korosho hana budi kuanza kulipa malipo
ya awali kabla ya kuingia kwenye mnada ili tuwe na uhakika wa kununua
korosho hizo na kuwalipa wakulima kwa wakati,” alisema.
Akizungumzia kuhusu changamoto ya
kushuka kwa uzalishaji wa korosho Waziri Mkuu aliutaka mfuko wa wakfu
wa kuendeleza zao hilo ufanye utafiti wa kubaini sababu ili waweze
kutafuta namna ya kuipatia ufumbuzi.
“Nitakuja kukutana na viongozi wa
mfuko waniambie wanafanya nini na wamefanya nini miaka mitatu iliyopita
na wana mpango gani huko mbele tunakokwenda kama hakuna mpango
tutauangalia mara mbili mbili kwani wana fedha nyingi lakini hata mbegu
hawapeleki kwa wakulima,” alisema.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu
aliitaka Bodi ya Korosho kuhakikisha kila msimu wakulima wanapata
pembejeo bora na zinawafikia kwa wakati ili waweze kupata mazao ya
kutosha.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi Ruangwa kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja uliopo kwenye kata ya Nachingwea mjini Ruangwa Julai 16, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Lindi , Renather Mzinga ambaye amepandishwa cheo na kuwa Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Lindi Julai 16,2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi, viongozi na baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Mtwara kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo Julai 16, 2016. Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo, Halima Dendego na wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi.
Baadhi ya Watumishi , Viongozi na wananchi wa mkoa wa Mtwara wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa huo Julai 16, 2016.
Post a Comment