Wizara ya Afya yazuia Matumizi ya Bidhaa za Tumbaku
Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inampongeza Mheshimiwa
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kupiga marufuku matumizi ya Shisha na uvutaji wa Sigara hadharani kama afua ya kupunguza
madhara ya tumbaku na madawa ya kulevya katika jamii.
Uchunguzi
wa kitalaam uliofanyika umebaini kuwa Shisha
ina madhara kwa afya ya watumiaji hasa vijana na watoto. Watumiaji wa Shisha wanatumia kiwango kikubwa cha
tumbaku kwa muda mfupi, hali inayoongeza madhara yatokanayo na tumbaku kama
vile: - Saratani, Magonjwa ya Mapafu, Kibofu cha mkojo, Tezi dume, Koo, Mdomo na
Kiywa, Ngozi, Ini, Ubongo.
Pia
imebainika kwamba matumizi ya Shisha huambatana
na kuongezewa dawa nyingine za
kulevya na hivyo hufanya watumiaji wa Shisha
kupata uraibu wa dawa za kulevya. Matumizi ya dawa hizo za kulevya ni kosa la
jinai.
AGIZO
Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inapenda kurejea na kusisitiza agizo lake la tarehe
12 Machi 2015 la kuzuia matumizi ya sigara na matumizi ya bidhaa za tumbaku katika maeneo ya umma.
Inakumbushwa
kwamba agizo hili limezingatia utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Bidhaa za
Tumbaku, Sura ya 121 T.L 2002, ya Sheria za Tanzania kipengele cha 12 (1)
ambacho kinakataza matumizi ya Tumbaku katika Maeneo ya Umma.
MADHUMUNI
Madhumu
ya Agizo hili ni kuilinda Jamii kwa ujumla kutokana na madhara yatokanayo na
moshi wa sigara. Wizara inawakumbusha wananchi wanaotumia bidhaa za tumbaku
kupunguza au kuacha kabisa matumizi ya tumbaku. Aidha, agizo hili linaijumuisha
jamii yote katika kubaini madhara ya tumbaku na umuhimu wa kuzuia matumizi ya
tumbaku katika maeneo ya kazi na maeneo yote ya umma.
WALENGWA
Agizo
hili linawahusu wananchi wote nchini wanaopata huduma katika maeneo ya umma
kama ilivyotafsiriwa na sheria husika.
MAENEO HUSIKA
Matumizi
ya tumbaku hayaruhusiwi katika maeneo yote ya umma. Maeneo haya yanajumuisha
ofisi zote za Serikali na tasisi zake zote, watu binafsi, vyuo, vituo vya
huduma za Afya zikiwemo Hospitali, vituo vya Afya na zahanati, vituo vya
usafiri wa Anga, Mabasi, bandari na treni, sehemu za mikutano, mapumziko,
bustani na fuko za maji,sherehe,michezo,masoko,maduka makubwa pamoja na sehemu
za kuabudu.Na kwa mtu yeyote anayeendesha shughuli katika maeneo ya umma
analazimika kutenga eneo maalum kwa ajili ya wavuta sigara.
UTEKELEZEJI
Kwa
kuwa Mhe. Waziri mwenye dhamana na masuala ya Afya nchini ameona hatari hii ya
Uvutaji wa sigara na utumiaji wa bidhaa za tumbaku kwa afya ya Wananchi, kuanzia
leo tarehe 4/7/2016 matumizi ya Shisha
nchini yamepigwa marufuku kwa wote wanaojihusisha na matumizi hayo, na kwa
wafanyabiashara wote wanaojihusisha na upatikanaji wa Shisha nchini.
Hivyo
basi, kwa agizo hili katika maeneo yote nchini ambako matumizi ya Shisha hufanyika ni marufuku matumizi hayo
kuendelea kutumika.
Aidha
vyombo vya Dola na mamlaka husika vinahimizwa kusimamia kwa ukamilifu katazo
hili.
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na
watoto – Afya
04/07/2016
Post a Comment