Meneja wa Wakala wa
Barabara nchini (TANROADS) mkoa wa Lindi Eng. Isaac Mwanawima akitoa taarifa ya
utendaji wa Wakala huo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa
Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto) wakati alipotembelea wakala huo.
Katika
hatua nyingine Waziri Mbarawa amemuagiza Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Eng. George Sambali kukamilisha kazi ya
kupima eneo la kiwanja cha Kikwetu ili kupata hati miliki na kudhibiti uvamizi
wa kiwanja hicho.
“Kama
kiwanja hiki hakitapimwa watu watavamia eneo la kiwanja na Serikali italazimika
kuingia gharama za kulipa fidia hivyo kuchelewesha maendeleo ya uwanja huo”,
amesema Prof. Mbarawa.
Ameongeza
kuwa Serikali iko kwenye hatua za mwisho za kutafuta fedha kwa kushirikiana na
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ili kuimarisha miundombinu ya kiwanja hicho
na kuongeza chachu ya maendeleo Mkoani
humo.
Naye
Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Kikwetu, mkoani Lindi Bw. Boniface Njanda amemuhakikishia
Waziri Prof. Mbarawa kuwa Mamlaka itafanya tathmini ya Kiwanja hicho kabla ya
kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami.
Waziri
Mbarawa yupo katika ziara ya kukagua utendaji kazi kwa wafanyakazi wa taasisi
zilizopo chini ya Wizara na kuangalia maendeleo ya utekelezaji wa miradi katika
kanda ya kusini.
|
Post a Comment