Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwakilishi maalum wa Masuala ya Maji
kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na
Rais Mstaafu wa Kenya Mhe. Mwai Kibaki wakati wa Ufunguzi wa Maadhimisho ya
Sita wa Wiki ya Maji ya Afrika, leo Jijini Dar es Salaam.
Akitolea
mfano, Waziri Mkuu alisema kuwa kupitia Ziwa Victoria, Tanzania inapakana na
nchi za Uganda na Kenya, Ziwa Nyasa na Malawi pamoja na Msumbiji, na Ziwa
Tanganyika Tanzania inapakana na Zambia pamoja na Jamhuri ya Demokrasia ya
Kongo, ambapo vyanzo hivyo vya maji vinaweza kutumika kuwahudumia watu wa
maeneo hayo kwa manufaa ya maendeleo ya sekta mbalimbali.
Aidha,
Waziri Mkuu Majaliwa amesisitiza kuwa wananchi wanaoishi karibu na vyanzo vya
maji wavitunze ili wananchi wanaotegemea vyanzo hivyo waendelee kupata huduma
ya maji endelevu kwa matumizi mbalimbali.
Akizunguzia
namna Tanzania inavyoshiriki mkutano huo, Waziri wa Maji na Umwagiliaji
Mhandisi Gerson Lwenge amesema kuwa malengo ya Tanzania ni kuhakikisha kufikia
mwaka 2020, Serikali imedhamiria kufikisha maji katika maeneo yote nchini
ambapo kwa upande wa vijijini inatarajiwa kufikia asilimia 85 na asilimia 95
kwa upande wa mijini.
Waziri
Lwenge ameongeza Serikali imejipanga na kuipa Sekta ya Maji kipaumbele, ambapo
katika bajeti ya mwaka huu zimetengwa zaidi ya Sh. trilioni 1 na hadi kufikia
2030 Tanzania itakuwa imekamilisha miradi yote ya maji kwa asilimia 100. Hayo
yakiwa ni malengo ya nchi za Afrika ya kuwapatia wananchi wote mijini na
vijijini maji kwa asilimia 100 hadi kufikia mwaka 2030.
|
Post a Comment