Watoto 13,266 mkoani TANGA kunuifaika na Huduma za Afya
Lee Kwiwoon akuzungumza na washiriki wa mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo vijana(Keepers) katika vijana waliofundishwa kuhudumia watoto katika masuala ya Afya na Lishe. |
Washiriki wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika mafunzo hayo. |
JUMLA
ya watoto 13,266 wenye umri chini ya miaka 10 wamenufaika mkoani hapa
na huduma za afya zitolewazo na taasisi ya Kikorea ijulikanayo kama
UHIC (United Help for International Children) .
Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi hiyo kanda ya Tanzania, Lee Kwiwoon alitoa taarifa
hiyo hapa mwishoni mwa juma lililopita katika mkutano uliojumuisha
madaktari, manesi na wahudumu wa afya kutoka wilaya tatu za mkoa huu,
ambazo zimelengwa katika mradi wa taasisi hiyo.
Mkurugenzi
huyo alisema lengo la kuanzisha taasisi hiyo ni kutoa huduma kwa watoto
wenye matatizo mbalimbali ya kiafya yanayowapata wenye umri chini ya
miaka 10.
Aliwaeleza
wanasemina hao kwamba watoto wengi walio katika umri chini ya miaka 10
hukumbwa na magonjwa mengi, hasa malaria, upungufu wa damu na utapiamlo.
Magonjwa mengine ni pamoja na kifua, kuzaliwa njiti na
kuharisha.
Lee
aliwaambia maofisa na manesi pamoja na wahudumu wa afya kwamba jukumu
kubwa la taasisi yake ni kuzuia magonjwa yanayowanyemelea zaidi watoto
wadogo pamoja na kuhakikisha watoto hao wanakua katika afya
bora.
Alifahamisha
kwamba taasisi hiyo ya UHIC imeanzisha mradi ujulikanao Keepers' ambao
unawafundisha na kuwapatia mafunzo vijana wanaotoa huduma ya kuokoa
maisha ya watoto kutoka janga la njaa, maradhi na kuwasaidia waishi
katika mazingira mazuri ya kiafya.
"Afya
na uzuiaji wa magonjwa yawapatayo watoto wengi mkoani Tanga ni suala
linalozungumzika na hivyo kuwafanya wadau kuamua kujitolea kuanzisha
taasisi zitakazosaidia kuondoa adha hiyo kwa watoto wetu", alisema
Lee.
Mkurugenzi
huyo alibanisha kuwa taasisi ya UHIC ni ya kimataifa iliyoanzishwa kwa
lengo la kutoa huduma endelevu za afya kwa watoto waishio maeneo ya
vijijini (pembezoni) mkoani hapa.
Alisema
wamechagua wilaya tatu ambazo ni Pangani, Muheza na Tanga kuwa za mfano
katika kuanza na mradi huo ambapo jumla ya vijiji 27 vitahusika.
Alisema taasisi yake ina jukumu la kugawa dawa na kwamba wahudumu 24
tayari wamekwishapatiwa mafunzo ya kuhudumia watoto hao katika vijiji
husika.
Akizungumza
katika mkutano huo, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa, Dkt. Rehema Maggid
alisema mkoa umepoteza maisha ya watoto wapatao 653 kutokana na magonjwa
mbalimbali, yakiwemo malaria, kikohozi, upungufu wa damu na
kuharisha.
Pamoja
na kupongeza msaada huo wa Korea akisema kuwa umefika wakati
ukihitajika sana, lakini akataka wataalamu wanaopelekwa kwenye vijiji
hivyo wapewe ushirikiano unaofaa.
Mapema,
akifungua semina hiyo, Kaimu Mkuu wa Mkoa waTanga, Mayassa Hashim
alisikitishwa na vifo hivyo ambapo alisema vingeweza kuzuilika kwa kutoa
elimu ya kutosha kwa wazazi .
Hata hivyo, Mayassa
ambaye pia ni OfisaElimu wa Mkoa, alieleza matumaini kwamba ujio wa
taasisi hiyo pamoja na madawa na wataalamu wao itasaidia kuondoa vifo
visivyotarajiwa vya watoto wadogo.
Post a Comment