Header Ads

Wadau wa Sanaa Watakiwa Kuwasaidia Wasanii Wanaochipukia

Na Shamimu Nyaki WHUSM

Serikali imewataka wadau wa kazi za sanaa kuwasaidia wasanii wachanga katika kazi zao ili waweze kufanikiwa na kutangaza kazi zao  kimataifa.

Wito huo umetolewa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi.Joyce Fissoo jijini Dar es Salaam wakati akimkabidhi Bi Wakonta Kapunda Shilingi laki tano kwa ajili ya Safari ya kwenda Zanzibar kushiriki mashindano ya uandishi wa Muswada (Script).

“ Napenda kutoa wito kwa wadau wa sanaa kusaidia wasanii wanaochipukia kwani ni nguzo muhimu kwa maendeleo ya sanaa nchini” Alisema Bi Joyce.

Kwa upande wake Bi Wakonta Kapunda ametoa shukrani kwa watanzania wote ambao wamejitoa kwa ajili ya kufanikisha safari yake na bado wamekuwa watu wa karibu kwake katika kufanikisha ndoto yake ya kuwa mwandishi bora wa Muswada.

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akisalimiana na Bw. Bazilio Kapunda baba wa Wakonta wakati wa kukabidhi msaada wa shillingi laki 5 kwa Wakonta Kapunda ambaye ni mshiriki wa mashindano ya uandishi wa muswada wa filamu yatayofanyika Zanzibar.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akizungumza wakati wa kukabidhi msaada kwa wa shillingi laki 5 kwa Wakonta Kapunda ambaye ni mshiriki wa mashindano ya uandishi wa muswada wa filamu yatayofanyika Zanzibar.

“Naweza kusema kuwa mimi ni mtu mwenye bahati kwani nimekuwa nikipata msaada  kutoka kwa  watu mbalimbali wananipigia simu na kunipa faraja lakini najua kuna wengi wapo kama mimi na wamesahaurika hawana msaada “Alisema Bi Wakonta.

Naye Bw. Bazilio Kapunda baba wa Wakonta ameishukuru Bodi ya Filamu Tanzania na wadau wa Filamu nchini kwa msaada mkubwa kwa mtoto wake na kuwaasa wadau wa sanaa nchini kuendelea kusaidia wasanii wanaochipukia.

Wankota Kapunda ni mwandishi wa muswada wa filamu anayechipukia ambaye alipata ajali ya gari mwaka 2012 akiwa kidato cha sita katika shule ya sekondari ya wasichana Korogwe na kupooza mwili mzima, yupo Zanzibar kushiriki katika warsha ya uandishi wa Muswada (Script) iliyoandaliwa na Maisha Film Lab baada ya kuibuka mshindi kati ya washindi wa Muswada (script) 15 baada ya script yake kuibuka mshindi Julai 5, 2016.
Wakonta Kapunda akimshukuru Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo kwa msaada wa shillingi laki 5 ambaye ni mshiriki wa mashindano ya uandishi wa muswada wa filamu yatayofanyika Zanzibar.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akikabidhi msaada wa shillingi laki 5 kwa Wakonta Kapunda ambaye ni mshiriki wa mashindano ya uandishi wa muswada wa filamu yatayofanyika Zanzibar, Jijini Dar es Salaam.

No comments

Powered by Blogger.