Na Shamimu Nyaki WHUSM
Serikali imewaasa Vijana nchini kujiajiri kupitia filamu kwakua ni Sekta ambayo inatoa nafasi kubwa kwa kundi hilo lenye uhitaji mkubwa wa ajira hapa nchini.
Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi Joyce Fissoo alipokuwa akitoa mafunzo kwa Vijana kuhusu Umuhimu wa Sekta ya Filamu katika kutoa ajira kwa vijana.
Amesema kuwa Sekta ya Filamu ni Sekta ambayo inaweza kusaidia vijana kujiajiri kwa kuwa ina vipengele vingi vinavyoweza kuwasaidia ikiwemo uandishi wa Mswaada, utengenezaji wa Filamu, uigizaji, upigaji picha na kuhariri.
“Takribani asilimia 70% ya watu wamepata ajira kupitia filamu hivyo ni vyema na nyie mkatumia elimu mnayopata hapa na vipaji vyenu kufanya filamu ili kujikomboa kiuchumi”Alisema Bi Joyce.
Ameongeza kuwa ni vyema Vijana kuwa wazalendo kwa kutengeneza Filamu ambazo zitakuwa na maadili ya kitanzania ambazo zitakuwa zinatazamwa na kila mtu bila kujali umri kwakua Filamu mbali ya kuelimisha pia inatoa burudani.
|
Post a Comment