Header Ads

UN yashinda Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Saba Saba


Shirika la Umoja wa Mataifa limenyakua tuzo ya mwoneshaji bora kwenye kategori ya habari, machapisho, uchapishaji na vifaa vya ofisini katika sherehe za uzinduzi wa maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.

Tuzo hiyo imekabidhiwa na mgeni rasmi Rais wa Rwanda Mh. Paul Kagame na kupokelewa na Mkuu wa Masharika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Bw. Alvaro Rodriguez.

Umoja wa Mataifa umekuwa kinara wa kuelimisha wananchi, kupitia njia mbalimbali ikiwemo redio, magazeti mitandao ya kijamii na pia kushiriki katika maonyesho ya sabasaba kila mwaka kwa Zaidi ya miaka 6 na kwa miaka 5 mfululizo wamekuwa wakishinda tuzo hizo.

Umoja wa Mataifa mwaka huu umekuja na kampeni ya uhamasishaji wa Malengo ya dunia (Global Goals) na umuhimu wa watanzania kuyaelewa malengo hayo na kuwa mabalozi katika kuhakikisha malengo hayo mapya ya maendeleo endelevu (SDGs) yanatekelezeka.

Banda la Umoja wa Mataifa linapatikana katika ukumbi wa Karume yanakoendelea maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa almaarufu 'sabasaba' katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Rais wa Rwanda Paul Kagame, (wa pili kulia) akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli, (wa kwanza kulia), akimkabidhi tuzo ya mwoneshaji bora kwenye kategori ya habari, machapisho, uchapishaji na vifaa vya ofisini, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Bw. Alvaro Rodriguez, wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Julai 1, 2016. Wapili kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mh. Charles Mwijage.

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Bw. Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wakiwa na tuzo ya ushindi katika banda lao. Kulia Felister Bwana wa Shirika la UNFPA Tanzania, Didi Nafisa (wa pili kulia) pamoja na Hoyce Temu (kushoto).

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Bw. Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wakiwa na tuzo ya mwoneshaji bora kwenye kipengele cha habari, machapisho, uchapishaji na vifaa vya ofisini katika banda lao. Kulia Felister Bwana wa Shirika la UNFPA Tanzania, Didi Nafisa (wa pili kulia), Hoyce Temu (katikati) pamoja na Edgar Kiliba (kushoto).

Wataalamu wa mawasiliano na Uhamasishajii (Communications, Advocacy and Partnership-COAP) wa ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini wakifurahia ushindi huo katika banda lao. Kutoka kushoto ni Edgar Kiliba, Hoyce Temu na Didi Nafisa.

No comments

Powered by Blogger.