Taasisi ya METDO yahimiza Wazee Wanaolelewa Kituo cha BUKUMBI kusaidiwa
Ashraph Omary (wa pili kushoto) akizungumza jambo kwa niaba ya Wanachama/Wafanyakazi kutoka Taasisi ya METDO (Mining and Environmental Transformation For Development Organisation, walipotembelea Kituo cha Wazee Bukumbi kilichopo Misungwi mkoani Mwanza.
Wafanyakazi wa METDO wakiambatana na Mwenyekiti wa Chama cha Madereva wa daladala Kanda ya Ziwa, Hassan Dede pamoja na Wanafunzi wa Geita International School, waliwakabidhi wazee wanaolelewa katika kituo hicho msaada wa mahitaji mbalimbali ikiwemo chakula.
Taasisi ya METDO kupitia kwa msemaji wake, Ashraph Omary, iliwahimiza wanajamii kwa kushirikiana na taasisi za serikali na binafsi kuwasaidia wazee wanaoishi katika kituo hicho ili kuondokana na changamoto zinazowakabiri ikiwemo ukosefu wa mavazi, chakula, matibabu pamoja na ujenzi wa uzio kituoni hapo ikiwa ni miongoni mwa changamoto zilizoanishwa kuwakabiri wazee hao.
Pichani Baadhi ya Wazee wanaolelewa katika Kituo hicho Jijini MWANZA.
Post a Comment