Na Catherine Sungura, Muleba Serikali inatambua na kuthamini mchango wa hospitali za mashirika ya dini katika kutatua matatizo ya wananchi nchini.
Hayo yamesema jana na waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu alipotembelea hospitali teule ya wilaya ya Rubya iliyopo wilayani Muleba
"Sera ya afya ni ileile hivyo tutaendelea kushirikiana katika kuboresha huduma zinazotolewa na madhebebu ya dini,hivyo bado ipo haja ya kufanya kazi nanyi"alisema
Waziri ummy alisema licha ya changamoto kubwa ya watumishi,wizara yake itaendelea kuwapangia watumishi katika hospitali hizo bila kudhoofisha utendaji wao
Alisema upungufu wa watumishi katika sekta ya afya nchini ni asilimia 48 ila kwa mkoa wa kagera upungufu ni asilimia 54,hivyo mkoa una uhaba mkubwa wa watumishi katika sekta ya afya.
|
Post a Comment