Serikali yaipongeza SBL kwa Uhifadhi wa Mazingira
Mheshimiwa Luhaga Mpina Naibu waziri ofisi ya makamu wa raisi mazingira (katikati) akiongozana na Mhe. Mbunge wa Temeke , Abdallah Mtolela (kushoto) na Meneja wa mradi wa kusafirisha maji taka wa kampuni ya bia ya Serengeti Bwana Peter Mkongwa wakiongozana kuelekea kwenye mtambo wa kusafirisha majitaka kiwandani hapo.
Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya bia ya Serengeti, John Wanyancha akifafanua jambo wakati ya ziara ya Mhe. Luhaga Mpina Naibu waziri ofisi ya makamu wa raisi mazingira alipotembelea kuona ujenzi wa mtambo wa kusafirisha majitaka kiwandani hapo pamoja na namna kiwanda kinavyofanya shughuli zake kwa kuzingatia sera za mazingira. |
Kampuni ya bia ya Serengeti leo imepongezwa na serikali kwa juhudi zake za uhifadhi wa mazingira na kutajwa kuwa mfano mzuri wa mashirika binafsi yanayoounga mkono jitihada za kulinda mazingira nchini.
Haya yamesemwa leo na naibu waziri katika ofisi ya makamu wa rais, anayeshughulika masuala ya mazingira na muungano, Luhaga Mpina, alipofanya ziara ya ukaguzi wa mazingira katika kiwanda cha SBL kilichoko Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Katika ziara hiyo naibu waziri alijionea harakati mbalimbali zinazofanywa na SBL katika uhifadhi wa mazingira ikiwemo ujenzi wa bomba maalum lenye urefu wa kilomita 2.1 linalosafirisa majitaka kutoka kiwandani hapo hadi mfumo wa majitaka wa DAWASCO ulioko kurasini.
“Napenda kuipongeza sana kampuni ya SBL kwa ujenzi wa bomba hili la majitaka ambalo tunaamini litasaidia katika kuendeleza kuimarisha usafi na uhifadhi wa mazingira katika kiwanda hiki na pia kwa jamii inayokizinguka.
Mpina aliongozana na mbunge wa Temeke Abdalla Mtolea, ujumbe kutoka Baraza la Mazingira (NEMC) na uongozi wa juu wa halmashuri ya wilaya ya Temeke.
Akitolea ufafanuzi ujenzi wa mfumo huo wa majitaka, Mkurugenzi wa Mahusiano wa SBL John Wanyancha amesema kampuni hiyo imetumia zaidi ya shilingi 470 kukamilisha mradi huo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya SBL ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira.
“Bomba hili la usafirishaji wa majitaka ni kielelezo cha jinsi ambavyo SBL inajali na kulinda mazingiar kwa manufaa mapana ya jamii yetu na ustawi wan chi ya Tanzania,” alisema Wanyancha akisema kwamba majitaka yanayosafirishwa na bomba husafishwa kwanza kiwandani kabla ya kuelekezwa kwenda kwenye mfumo wa majitaka wa DAWASCO.
Post a Comment