Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi mara baada
ya kuwasili katika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya Baraza la Eid El fitri.
Aidha Rais
Magufuli amezungumzia juhudi zinazofanywa na BAKWATA katika kuimarisha taasisi
zake zinazotoa huduma za kijamii na kulinda mali zake akisema serikali itahakikisha
mali zote za waislamu zinakuwa salama na kwamba wote waliodhulumu mali za
waislamu watazirejesha.
Awali akisoma
taarifa, Katibu Mkuu wa BAKWATA Alhaji Suleiman Said Lolila amesema BAKWATA
inakusudia kupanua huduma za kijamii kwa lengo la kuwahudumia wananchi ikiwemo
kujenga chuo kikuu Mkoani Dodoma na pia amempongeza Rais Magufuli kwa juhudi
zake za kuondoa umasikini huku akimtaka asikatishwe tamaa na wachache
watakaoudhika kwa kuguswa na hatua zinazochukuliwa.
Nae Mufti wa
Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Ali pamoja na kumshukuru Rais Magufuli kwa
kuongoza bila ubaguzi amewataka watanzania kuungana na juhudi za serikali
kupinga matendo maovu ikiwemo rushwa na ufisadi na pia amelaani ndoa za jinsia
moja akisema ni kinyume na maadili ya dini.
Baraza la Eid
el-Fitr pia limehudhuriwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Rais Mstaafu wa
awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi, mabalozi na wabunge.
|
Post a Comment