Mkuu wa Wilaya ya Handeni GODWIN GONDWE ataka Wafanyabiashara Kuwekeza Kwenye Kilimo
MKUU wa wilaya ya Handeni Mkoani
Tanga,Godwin Gondwe amewataka wafanyabiashara kuhakikisha wanawekeza
kwenye kilimo kikubwa cha kisasa ambacho kitakuwa na tija kwao ili
kuweza kusukuma gurudumu la maendeleo na kukuza uchumi.
......................
Gondwe alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na
wafanyabiashara, viongozi wa dini ambapo pamoja na mambo mengine
aliwataka kuona umuhimu wa kutumia fursa ya uwepo wa rutuba nzuri ya
ardhi iliyopo wilayani humo kujikita kulima kisasa ili kuweza kupata
mafanikio.
Alisema kuwa lazima wafanyabiashara watambue kuwa kilimo ndio njia pekee
ambayo inaweza kuwainua kiuchumi na kuharakisha kasi ya ukuaji wa
maendeleo iwapo watazingati na kukipa kipaumbele kila wakati
“Niwaombeni suala la kilimo mlipe msukumo mkubwa sana
kwani hii ndio
njia pekee ambayo inaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kusukuma gurudumu
la maendeleo kwa wilaya yetu “Alisema.
Aidha pia alisisitiza umuhimu wa wananchi wa wilaya hiyo kutilia mkazo
kulima mazao yanayostahimili ukame ikiwemo Alizeti, Ufuta,Viazi na
Mihogo ili kuweza kukabiliana na tatizo la kutoku patikana mvua za
uhakika kwa ajili ya kilimo cha mahindi.
“ Ninajua katika kipindi hiki tumelima kwa wingi lakini hali ya hewa
sio nzuri na mvua nazo zimekuwa hazipatikana kwa uhakika hivyo lazima
wakulima tubadilike kwa kuanza kupanda mazao yanayostahimili ukame ili
kuweza kuepukana na baa la njaa “Alisema DC Gondwe.
Sambamba na hayo,Mkuu huyo wa wilaya alizishauri taasisi za kibenki
wilayani humo kuhakikisha zinatoa kipaumbele kwa wawekezaji wa kilimo
ili waweze kuzalisha kwa wingi mazao ambayo yataweze kuinua kiuchumi
lakini pia kuchangia pato la Taifa.
Hata hivyo ,Mkuu huyo wa wilaya alitumia pia fursa hiyo
kuwaasa
wakulima waliopata mazao kidogo kuhakikisha wanayatunza na kuacha
kuyauza kwani kufanya hivyo kutaweza kusababisha hali ya njaa
kwao
Naye Sherhe wa wilaya ya Handeni, Shabani Mohamed alisema kuwa wao
watamuombea dua Mkuu huyo wa wilaya ili mungu amuwezeshe kuweza kutimiza
majukumu yake ipasavyo na kusaidia kuchangia juhudi za maendeleo kwa
wananchi.
“Nikuambie Mh Mkuu wa wilaya ujio wako hapa Handeni watu wengi
wamefurahi sana kwani uchapakazi wako unafahamika tokea ulipokuwa
unafanya kazi kwenye kituo cha ITV na tunaamini uhodari huo pia
utasaidia kuinua uchumi wetu “Alisema.
Alisema kuwa wao watahakisha wanampa ushirikiano wa hali ya juu ili
kumuwezesha kutekeleza vema majukumu yake ya kuipa maendeleo wilaya
hiyo.
Post a Comment