Kongamano la Vijana Wajasiriamali na Wawekezaji lafana Jijini MWANZA
Mgeni Rasmi, Meneja wa Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo SIDO mkoani Mwanza, Damian John Changa, akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Biashara, Viwanda na Uwekezaji, katika ufungaji wa Kongamano la Vijana Wajasiriamali na Wawekezaji mkoani Mwanza lililohitimishwa jana katika Viwanja vya Gandh Hall Jijini Mwanza.
Alisema umefika wakati wa vijana kuacha kuilalamikia Serikali huku wakiwa hawajishughulishi katika kujipatia kipato hivyo kongamano hilo anaamini limewafungua vijana wengi mkoani Mwanza ambao watatumia elimu ya ujasiriamali na uwekezaji waliyoipata kutumia fursa zilizopo mkoani Mwanza ili kujikomboa kiuchumi.
Kongamano hilo lilifanyika kwa siku mbili kuanzia jumamosi Julai 16,2016 hadi jana jumapili julai 17,2016 ambapo liliandaliwa na Taasisi ya Tanzania Youth Enterpreurship Organization pamoja na Taasisi ya Vijana Mwanza Saccos kwa lengo la kuwawezesha vijana kukutana pamoja kuzungumza, kujadili na kutathimini kwa pamoja fursa zilizopo mkoani Mwanza na kuzitumia ili kukabiliana na changamoto za kiuchumi.
Kauli mbiu ya Kongamano hilo ilikuwa ni "Kijana ndio Mhimili wa Upaishaji wa Pato la Taifa, Usisubiri kesho, Fursa ni Sasa".
Afisa Maendeleo ya Jamii Jijini Mwanza, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, katika hitimisho la Kongamano la Vijana Wajasiriamali na Wawekezaji mkoani Mwanza.
Mwenyekiti wa Kongamano la Vijana Wajasiriamali na Wawekezaji mkoani Mwanza, akizungumza katika hitimisho la kongamano hilo jana.
Alisema kongamano hilo limevunga lengo la kuwafikia vijana 1,100 kwani zaidi ya vijana 2,000 walihudhuria huku pia lengo la kuvifikia vikundi 50 vya wajasiriamali mkoani Mwanza likivukwa baada ya vikundi 150 kujiandikisha na kushiriki katika kongamano hilo.
Beatus Kisusi ambae alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Kongamano hilo akizungumza wakati wa ufungaji wake jana.
Florah Magabe ambae alikuwa mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano la Vijana Wawekezaji na Wajasiriamali mkoani Mwanza, alitanabaisha kwamba lengo ni kongamano hilo kufanyika katika mikoa mbalimbali nchini ili kuwafikia vijana wengi zaidi ili waweze kutumia fursa zilizopo katika kujikwamua kiuchumi.
Mdau wa Maendeleo Jijini Mwanza ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini, Jumanne Kishimba, akitoa Mada kuhusu "Watu waliopambana na Maisha na kufanikiwa katika harakati za kuzalisha mali".
Mh.Dkt.Antony Diallo ambae ni Mkurugenzi wa Sahara Media Group, akitoa mada juu ya "Ujasiriamali na Uwekezaji katika Mkoa wa Mwanza" katika kongamano la Vijana Wajasiriamali na Wawekezaji mkoani Mwanza.
Miongoni mwa watoa Mada katika kongamano hilo ambae alitoa mada juu ya "Umuhimu wa Bima katika Biashara".
Post a Comment