Naibu
Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh,Luhaga Mpina
akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ziara katika kiwanda cha
pepsi kilichopo kiwalani,temeke jijini dar es salaam.
Awali akitamka adhabu hiyo
Mkaguzi Mkuu wa Kanda ya Mashariki kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na
Usimamizi wa Mazingira NEMC Bw. Jaffari Chimgege alisema kuwa pamoja na adhabu hiyo kiwanda hicho cha Pepsi
pia kimekuwa na kosa la kutiririsha maji hayo machafu bila kuyatibu na kwa
mujibu wa sheria ya wenye viwanda walitakiwa kukusanya taarifa ya ukaguzi kwa
baraza, ili kuona kama wanatekeleza sheria ya mazingira na hawakufanya hivyo.
“Wafanyie kazi haraka taarifa ya ukaguzi.”
Kwa upande wake, Afisa Mauhusiano wa kiwanda hicho Bw.
Alexandra Nyirenda aliliomba Baraza (NEMC) kuelekeza wenye viwanda zaidi ya
mara mbili kabla ya kutoa adhabu, ili waweze kwenda sawa na utekelezaji wa Sheria ya mazingira na kanuni
zake kwani kujisahau ni ubinadamu.
Wakati huo huo; Mhe Naibu Waziri Mpina amezindua bomba lenye
urefu wa kilometa mbili la, utoaji maji taka katika kiwanda cha bia cha
Serengeti. (SBL) cha Chang’ombe Jijini Dar es Salaam.
|
Post a Comment