Afisa
Madini Mkazi Dodoma, Mhandisi Slimu Mtigile (katikati) akiwa na wamiliki wa
mgodi wa Mawe ya Nakshi wa Ntyuka.
Alisema
soko la mawe hayo kwa nchi za Ulaya, China na Japan ni kubwa na hivyo malengo
na matarajio yao ni kuhakikisha wanazalisha bidhaa yenye ubora wa hali ya juu
ambayo itakubalika katika nchi hizo na vilevile nchi zingine zitakazokuwa na
uhitaji.
“Wazalishaji
wengi wa mawe ya nakshi hapa nchini soko lao ni hapa hapa lakini sisi tumelenga
kwenda hadi nje ya Tanzania; tunatarajia kuwa na uzalishaji wenye kiwango cha
kimataifa,” alisema Nayak.
Alisema
kiwanda hicho vilevile kitahudumia wachimbaji wadogo wa madini ya aina hiyo wa
maeneo jirani ili nao waweze kupata bidhaa zenye ubora na hivyo kujiongezea
kipato kutokana na shughuli husika.
“Kiwanda
chetu kitapokea kazi kutoka kwa wachimbaji wadogo wa mawe ya nakshi na ili
kuwasaidia kuinua kipato chao, tutatoza gharama nafuu,” alisema Nayak.
Akizungumzia
makadirio ya gharama za shughuli za uchimbaji wa madini hayo hadi ujenzi wa
kiwanda, Nayak alisema mradi huo kwa pamoja unatarajiwa kugharimu kiasi cha
Dola za Marekani milioni 5.5.
Aidha,
alisema shughuli za uchimbaji wa awali wa madini katika mgodi huo zilianza
mwezi Mei mwaka huu na kwamba uzalishaji rasmi unatarajiwa kuanza mwezi Oktoba
mwaka huu mara baada ya kukamilika kwa vifaa vya uchimbaji ambavyo vinatarajiwa
kuwasili hivi karibuni kutokea nchini India.
Naye
Mhandisi Mtigile alipongeza juhudi zinazofanywa na mgodi huo katika utekelezaji
wa shughuli zake na kuuasa kuhakikisha unafuata sheria za zilizopo ili kuwa na
uzalishaji wenye tija.
“Ili
mfanye shughuli zenu kwa ufanisi bila usumbufu, hakikisheni mnafuata sheria,
taratibu na kanuni zilizopo na endapo mtakutana na vikwazo vya aina yoyote
Ofisi yetu ipo wazi kutoa ushirikiano,” alisema.
Alisema
uanzishwaji wa mgodi huo pamoja na ujenzi wa kiwanda husika utakuwa na mchango
mkubwa katika kuinua uchumi wa wananchi wa maeneo jirani na vilevile kuongeza
pato la Taifa kutokana na kodi na tozo mbalimbali za Serikali.
Aidha,
alitoa wito kwa wachimbaji wengine kuendesha migodi yao kitaalam ili kufaidi
matunda yatokanayo na shughuli zao za uchimbaji na vilevile kutoa ushirikiano
kwa Ofisi ya Madini kwa lengo la kuboresha shughuli zao.
|
Post a Comment