Header Ads

Hizi hapa Tetesi za Usajili kwenye Soka la ULAYA


Manchester United wamewaambia Juventus kuwa wako tayari kulipa pauni milioni 100 kumsajili kiungo kutoka Ufaransa Paul Pogba, 23, na watampa mshahara wa pauni 250,000 kwa wiki (Mail on Sunday).
Arsenal watampa mkataba mpya Arsene Wenger kwa matumaini ya kumshawishi asiondoke baada ya tetesi kuzagaa kuwa chama cha soka cha England, FA, kinamnyatia (Observer).
Meneja mpya wa Manchester City, Pep Guardiola anataka kumsajili mshambuliaji kutoka Uruguay anayeichezea Barcelona, Luis Suarez, 29, anayedhaniwa kuwa na thamani ya pauni milioni 85, pamoja na kiungo Mjerumani anayechezea Real Madrid, Toni Kroos, 26, ambaye kipengele chake cha uhamisho kina thamani ya pauni milioni 63 (Sunday Mirror).
Mabingwa wa Ufaransa Paris St-Germain wamekubali kumsajili kiungo kutoka Poland anayechezea Sevilla Gregorz Krychowiak, 26, kwa pauni milioni 22 (Marca).
Liverpool watapambana na Everton katika kumsajili kiungo kutoka Ubelgiji Axel Witsel, 27, anayecheza soka Zenith St Petersburg nchini Urusi (Sunday Mirror).
Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na Arsenal, Robin van Persie, 32, huenda akarejea katika ligi kuu ya England baada ya klabu yake ya sasa Fernabahce ya Uturuki kuwaambia West Ham na Crystal Palace kuwa wanaweza kumsajili (Sun on Sunday).
Chelsea wamefanikiwa juhudi za kumsajili beki kutoka Senegal, Kalidou Koulibaly, 25, anayechezea Napoli kwa pauni milioni 30 (Sunday Mirror).
Tottenham wanajiandaa kutoa pauni milioni 38, kumtaka mshambuliaji wa Inter Milan, Mauro Icardi, 23, na tayari wamepeleka wawakilishi wao Italy kuzungumza na mchezaji huyo kutoka Argentina (GianlucaDiMarzio), kipa wa Spurs Hugo Lloris, 29, ananyatiwa na Real Madrid kwa pauni milioni 35 (Sunday Mirror).
Meneja wa Tottenham, Mauricio Pochettino yuko tayari kumuuza Ryan Mason, 25, kwenda Hull City iliyopanda daraja kwa pauni milioni 10 (Sun on Sunday), kiungo wa Watford Jose Manuel Jurado, 30, amehusishwa na kuhamia Espanyol na kuungana na meneja wake wa zamani Quique Sanchez Flores (Fichajes).
Middlesbrough watakamilisha usajili wa pauni milioni 11.75 wa kiungo kutoka Atalanta, Marten de Roon, 25, baada ya kukubaliana maslahi binafsi na mkataba wa miaka minne (Gazette),
Timu nne za EPL zimekuwa zikiwasiliana na wawakilishi wa mshambuliaji wa Wales, Hal Robson Kanu tangu alipopachika bao dhidi ya Ubelgiji kwenye michuano ya Euro 2016.
Kanu ni mchezaji huru baada ya kuachiliwa na klabu yake ya Reading (Sky Sports).
Stoke huenda wakalazimika kulipa takriban pauni milioni 20 kama wanataka kumsajili mshambuliaji wa West Brom, Saido Berahino, 22 (Stoke Sentinel).

No comments

Powered by Blogger.