EPZA yatengeneza Ajira 36,000 kwa Watanzania
Ofisa Mwamasishaji Mwandamizi wa Mamlaka ya Maeneo Maalumu ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA), Nakadongo Fares (kulia), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu mambo mbalimbali yanayofanywa na mamlaka hiyo. Kushoto ni Meneja Uhamasishaji Uwekezaji, Grace Lemunge.
Meneja Uhamasishaji Uwekezaji, Grace Lemunge (kushoto), akisisitiza jambo kwenye mkutano huo na wanahabari.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Star Infrastructure Development (T) Limited, Ananth Bhat akizungumzia mradi wao wa uwekezaji uliopo mkoani Morogoro.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
MAMLAKA ya Maeneo Maalumu ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA) imeweza kutengeneza ajira 36,000 kwa watanzania kupitia makampuni 140 yaliyowekeza hapa nchini.
Hayo yamebainishwa na Ofisa Mwamasishaji Mwandamizi wa Mamlaka hiyo, Nakadongo Fares Dar es Salaam leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mambo mbalimbali yanayofanywa na mamlaka hiyo kwenye maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam 2016.
"Kupitia makampuni 140 yaliyowekeza hapa nchini yameweza kutoa ajira kwa watanzania 36,000 huku watoa huduma wakiwa 300,000" alisema Fares.
Alisema kazi kubwa ya mamlaka hiyo ni kuhasisha uwekezaji katika kanda maalumu za kiuchumi, kuvutia na kuhamasisha uhuishaji wa teknolojia mpya, kuhamasisha uwekezaji kwenye viwanda usindikikaji wa malighafi zinazopatikana nchini, kutengeneza fursa za ajira na kuongeza pato la fedha za kigeni nchi.
Post a Comment