Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam Kuongeza Muda wa Kufunga Maduka Makubwa ( SHOP MALLS)
Na Frank Shija, MAELEZO
Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam inakusudia kuruhusu baadhi
ya maduka makubwa kutoa huduma zaidi ya muda wa kawaida wa maduka kufungwa ili
kutoa fursa kwa wafanyakazi kupata huduma hiyo pindi wanapotoka makazini.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.
Paul Makonda alipomwakilisha Makamu wa
Rais kwenye hafla ya Futali iliyoandaliwa na Benki ya NMB jana jijini Dar es
Salaam.
Makonda alisema kuwa kusudio hilo linatokana na changamoto
ya upatikanaji wa nafasi ya kupata huduma hiyo kwa wafanyakazi kwani uchelewa kutoka maofisini jambo
lilalosababisha baadhi ya wafanyabiashara kupeleka bidhaa zao huko huko
ofisini.
Aliongeza kuwa amekusudia kufanya mambo muhimu matatu katika
kipindi hiki cha mwenzi mtukufu wa ramadhani ambapo aliyataja mambo hayo kuwa
ni kuongeza muda wa kufunga maduka hasa yale makubwa (malls), kupiga marufuku
uvutaji wa sigara katika maeneo ya umma na kupambana na watumiaji wa usafiri wa
pikipiki wanaokiuka sheria ya matumizi ya Kofia ngumu (helmet).
“Nimekusudia kufanya mambo muhimu matatu ndani ya mwezi huu
mtukufu wa ramadhan, niwadokeze tu kuwa mambo hayo ni pamoja na kuongeza muda
wa kufanya biashara kwa maduka makubwa (shopping
malls), kupiga marufuku uvutaji wa sigara katika maeneo ya umma na
kupambana na wavunjifu wa sheria ya matumizi ya helmet.” Alisema Makonda.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Tanzania
Bibi. Ineke Bussemaker alisema kuwa wao kama Taasisi ya Kifedha imekuwa na
desturi ya kuwajali wateja wao hivyo wanatumia fursa hii kushiriki pamoja na
wateja wao walio katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan ili kuwatia moyo
wakustahilifunga hiyo muhimu katika uislamu.
Aidha aliongeza kuwa NMB itaendelea kushirikiana na jamii
mbalimbali katika kuhakikisha inasaidia pale panapohitajika msaada wao kama
ambavyo wamekuwa wakitoa misaada katika kuchangia huduma za kijamii kama vile
madawati.
Post a Comment