Taasisi za Elimu zaombwa Kuwathamini Wahitimu waliofanya Vizuri
Wageni mbalimbali wakitembelea eneo la Vipimo na Mizani wakati wa hafla ya utoaji wa Tuzo na zawadi kwa wahitimu waliofanya vizuri katika masomo yao katika Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam. |
Baadhi ya wanafunzi na wahitimu wakitembelea mabanda ya maonesho. |
Mmoja wa Wahitimu wa CBE aliyefanya vizuri katika fani ya Rasilimali Watu Bi. Happyness Onani akipokea cheti kutoka kwa Mkuu wa Chuo hicho Prof.Emmanuel Mjema. |
Baadhi ya wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya utoaji wa Zawadi na kwa wahitimu iliyofanyika CBE kampasi ya Dar es Salaam.
Na Aron Msigwa - MAELEZO
Taasisi
za elimu kote nchini zimeaswa kujenga utamaduni wa kuthamini na
kutambua mchango wa wahitimu wanaofanya vizuri katika masomo yao
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa Chuo cha Elimu ya
Biashara Dar es Salaam (CBE) Prof.Emanuel Mjema wakati wa hafla ya
kuwatunuku vyeti na zawadi mbalimbali wahitimu wa chuo hicho takribani
20 waliofanya vizuri katika masomo yao kwa mwaka 2015.
Akizungumza
na jamii ya wanachuo na Wahitimu wa Zamani wa Chuo cha Elimu ya
Biashara na wale wanaofanya kazi katika maeneo mbalimbali nchini amesema
chuo chake kina utamaduni wa kuwatuza wahitimu wanaofanya vizuri katika
masomo yao kama motisha kuthamini juhudi zao ili kuhamasisha wengine
kufanya vizuri zaidi.
Amesema wahitimu 20 wa
fani mbalimbali zikiwemo za Rasilimali Watu,Uendeshaji wa Biashara,
Ununuzi na Ugavi, Vipimo na Mizani, Uhasibu, Ununuzi na Ugavi, Masoko
na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ngazi ya Stashahada,
Shahada,Diploma na Cheti wametunukiwa vyeti na kukabidhiwa zawadi
mbalimbali.
Prof. Mjema ameongeza kuwa mbali na
tuzo hizo wadau hao hususan wahitimu wa miaka ya nyuma wa chuo hicho
wapata fursa ya kujadili masuala mbalimbali ikiwemo kukijengea uwezo
chuo hicho pamoja na kuangalia shughuli za kitaaluma zinazofanyika.
"
Siku hii ni muhimu sana kwa Chuo cha Elimu ya Biashara, ni siku ambayo
tunathamini wahitimu wetu waliofanya vizuri kwa kuwapa Zawadi za vtu
mbalimbali kuthamini mchango na heshima waliokipa chuo chuo chetu"
Alisisitiza Prof.Mjema.
Ameongeza kuwa utoaji
wa zawadi na tuzo hizo unakwenda sambamba na na maadhimisho ya ya
Mahafali ya 50 ya chuo hicho kampasi ya Dar es Salaam yatakayofanyika
Novemba 12,2015 katika ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo mgeni rasmi
atakua Rais mstaafu wa awamu ya Pili Ali Hasani Mwinyi.
Akifafanua
kuhusu mahafali hayo ya 50 amesema kuwa wahitimu wapatao 2050 wa ngazi
mbalimbali watatunukiwa Shahada , Astashahada, Stashahada, shahada na
stashahada za Uzamili.
Kuhusu suala la nidhamu
chuoni hapo hasa mavazi amesema kuwa chuo chake kimeendelea kusisitiza
nidhamu na kuweka kanuni zinazowabana wanafunzi huku akifafanua kuwa
chuo hicho kilikua chuo cha kwanza kuweka sheria inayosimamia nidhamu ya
mavazi kwa wanafunzi.
Amesisitiza kuwa mavazi
ndiyo yanayompambanua mwananfunzi na kuonyesha tabia yake na kuongeza
kuwa nidhamu inapokua juu inawapa wanafunzi fursa nzuri ya kupata ajira
pindi wanapohitimu kwa kuwa tayari wanaaminika katika jamii.
Prof.Mjema
amebainisha hali ya nidhamu ya mavazi inaendelea kuzingatiwa kutokana
na Madhara ya kuzuiwanna kushindwa kuhudhuria vipindi wanayoyapata
wanafunzi waliokuwa wanakiuka kanuni na taratibu za chuo hicho
"Vijana
lazima wawe mfano wa kuiga na hawa ni wasomi ambao wanategemewa na
taifa, CBE imeshafukuza wengi kwa kukosa nidhamu, pia mwanafunzi
anayekosa maadili huathiri maendeleo ya chuo na wanafunzi wengine"
Amesisitiza.
Akizungumza kwa niaba ya wahitimu
wa zamani wa chuo hicho (Alumnae) Bw.Lusekelo Mwandemange amesema kuwa
wao kama wahitimu wanayo dhamana ya kuhakikisha maendeleo ya chuo
hicho yanapatikana.
Amesema wahitimu hao
wamekuwa kioo kwa jamii inayowazunguka kwa kuitumia elimu yao kutatua
changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii
Aidha
wameupongeza uongozi wa chuo hicho kwa kuendelea kuweka mazingira
rafiki ya kuwawezesha wanafunzi wa chuo hicho katika fani mbalimbali
kupata elimu yenye viwango ndani na nje ya nchi.
Pia wamesema kuwa wao kama wahitimu wameanzisha umoja wao utakaohusika kuchangia maendeleo ya chuo hicho.
Post a Comment