EWURA yawakutanisha wadau Jijini MWANZA kujadili Bei ya Maji
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Faisal Issa (Katikati) kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, akifungua Mkutano wa Wadau wa Maji uliofanyika jana Jijini Mwanza kati ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini
UWURA, Mamlaka ya Maji safi na MajiTaka Mkoani Mwanza MWAUASA na Wadau/Watumiaji wa Maji Jijini Mwanza kwa ajili ya kujadili ombi la MWAUASA kutaka kupandisha bei ya maji kuanzia mwezi January mwakani.
Na:George Binagi
Mwauasa inatarajia kupandisha bei ya maji kutoka wastani wa shilingi 669.00 kwa lita mita moja ya ujazo wa maji ambayo ni sawa na lita 1,000 hadi wastani wa shilingi 1,075.74 hiyo ikiwa ni kwa watumiaji wa majumbani na taasisi huku ujazo kama huo kwa matumizi ya kibiashara na Viwandani ikifikia wastani wa shilingi 1,62500.
Kulia ni Mhandisi Mutaekulwa Mutegeki akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu EWURA.
Kushoto ni Osward Mutaitina ambae ni Mjumbe wa Bodi EWURA.
Mkurugenzi Mkuu wa MWAUASA Mhandisi Antony Sanga akiwasilisha hoja za Mamlaka hiyo juu ya kupandisha bei ya maji. Hoja hizo ni pamoja na kuondokana na hasara ya gharama za uendeshaji za hivi sasa na hivyo kuiwezesha kukusanya mapato ambayo yatasaidia kuboresha utoaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi.
Mkutano wa Wadau wa Maji uliofanyika jana Jijini Mwanza kati ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini UWURA, Mamlaka ya Maji safi na MajiTaka Mkoani Mwanza MWAUASA na Wadau/Watumiaji wa Maji Jijini Mwanza kwa ajili ya kujadili ombi la MWAUASA kutaka kupandisha bei ya maji kuanzia mwezi January mwakani.
Mhandisi Thomas Mnunguli ambae ni Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma zinazodhibitiwa na EWURA akitoa maoni ya baraza hilo juu ya ombi la Mwauasa kutaka kuongeza bei ya huduma za maji.
Pamoja na mambo mengine, baraza hilo liliishauri Mwauasa kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato jambo ambalo litasaidia kutoa huduma bila kupandisha gharama ya maji.
Mkurugenzi wa EWURA Kanda ya Ziwa Mhandisi Nyirabu Musira akitoa mwongozo katika Mkutano wa Wadau wa Maji uliofanyika jana Jijini Mwanza kati ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini UWURA, Mamlaka ya Maji safi na MajiTaka Mkoani Mwanza MWAUASA na Wadau/Watumiaji wa Maji Jijini Mwanza kwa ajili ya kujadili ombi la MWAUASA kutaka kupandisha bei ya maji kuanzia mwezi January mwakani.
katika Mkutano wa Wadau wa Maji uliofanyika jana Jijini Mwanza kati ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini UWURA, Mamlaka ya Maji safi na MajiTaka Mkoani Mwanza MWAUASA na Wadau/Watumiaji wa Maji Jijini Mwanza kwa ajili ya kujadili ombi la MWAUASA kutaka kupandisha bei ya maji kuanzia mwezi January mwakani.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza John Wanga.
Diwani wa Kata ya Nyamagana Jijini Mwanza Biku Kotecha.
Mwakilishi kutoka Pespi Mwanza.
Mwakilishi kutoka Pepsi Mwanza.
Maoni kutoka kwa wakazi wa Jiji la Mwanza.
Maoni kutoka kwa wadau wa Maji Jijini Mwanza.
Hata hivyo baadhi ya wakazi wa Jiji la Mwanza wamependekeza Mwauasa kutathimini upya juu ya ongezeko la gharama za huduma ya maji kwa kulinganisha na mamlaka nyingine nchini ambapo EWURA itaendelea kupokea maoni ya wadau/watumiaji wa maji kwa muda wa wiki mbili kabla ya kutoa maamuzi yake hivyo wanatumiaji wa maji wanashauriwa kupeleka maoni yao katika ofisi za EWURA Zilizopo jengo la NSSF Ghorofa ya Jijini Mwanza.
Post a Comment