Dawasco yakana Kusambaza Maji yenye Kinyesi
DAWASCO YAKANUSHA KUSAMBAZA MAJI
YENYE KINYESI.
Mnamo
tarehe 08/11/2015 Magazeti ya Mzalendo na Majira yaliandika habari
zilizolenga upotoshaji na taharuki kwa
wananchi na hususa ni watumiaji wa Maji kwa mkoa wa Dar es salaam wanaohudumiwa
na DAWASCO.
Katika
gazeti la Mzalendo lilikuwa na kichwa cha habari “Wengi Dar watumia maji yenye kinyesi” na upande wa gazeti la Majira
lilibeba kichwa cha habari “Maji machafu
yaathiri Dar”. Ndani ya habari hizo waandishi wameelezea shirika la
Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO) kama moja ya chanzo cha ugonjwa wa
kipindupindu kwa kuwa maji hayo yameathirika na kinyesi.
Gazeti
la Majira 08/11/2015 ukurasa wa 3 inanukuliwa “Kwa kiasi kikubwa Maji ya jiji
yamekuwa yameathirika na kinyesi cha binadamu”. mwisho wa kunukuu. Aidha nukuu
nyingine kwenye gazeti la Majira inasomeka “Wananchi wa jiji la Dar es salaam
wamekuwa wakipata Majisafi na salama kutoka mamlaka ya Majisafi na salama
(DAWASCO) kwa aslimia 30 tu”.
Ikumbukwe pia maeneo makubwa ambayo wagonjwa wa
kipindupindu wanatoka ni maeneo ambayo yameathirika na wizi wa maji kwa kiasi
kikubwa na mapambano hayo bado yanaendelea kuhakikisha wizi wa maji unakwisha
maeneo hayo ni pamoja na Manzese,
Buguruni ,Kigogo , Mburahati , Kinondoni mkwajuni pamoja na Tandale.
Jitihada
zilizofanywa na Dawasco katika kudhibiti
ugonjwa huu hususa ni watumiaji Maji
ni pamoja na
·
Kupeleka huduma ya maji BURE kwa maeneo yaliyoathirika zaidi na
mlipuko huo kupitia utarartibu wa Manispaa uliowekwa.
·
Kutoa Elimu kwa wananchi kupitia vyombo
vya habari , machapisho, pamoja na vikao vya pamoja na watendaji wa Mitaa,
Bwana Afya kwa maeneo yaliyoadhirika.
·
Kuanza kwa usajili rasmi wa magari
yanayofanya biashara ya maji (water bowsers) ili kulinda afya ya mtumiaji. Zoezi lilianza tarehe 01 October 2015 na idadi ya Magari 120
yameshasajiliwa hadi sasa.
·
Kuondoa
maunganisho yasiyo halali ambayo yanafanywa na baadhi ya wananchi “vishoka” , ambayo yanapeleka huduma ya
Maji kwa baadhi ya maeneo yanayoadhirika zaidi.
Dawasco inasikitika kwa taarifa hizo za upotoshaji
kwani tangu kuibuka kwa ugonjwa wa Kipindupindu jitahada mbali mbali
zimefanyika kwa kushirikiana na Mamlaka husika ikiwemo Wizara ya Afya , Ofisi
ya Waziri Mkuu kitengo cha maafa ,kikosi cha kupambana na ugonjwa wa
kipindupindu katika Ofisi ya Mkuu wa mkoa na taaisi nyingine nyingi zenye
kutetea ustawi wa Afya ya Jamii.
Dawasco
inapenda kuwakumbusha vyombo vya habari kuzingatia weledi na utashi katika
kuteleza majukumu yao ya kila siku ili kuwapatia wananchi taarifa zilizo sahihi
na zenye ukweli siku zote.
Tunaamini
kosa la namna hiyo halitajirudia tena ili kuepusha adha na usumbufu kwa
wananchi kama ulivyojitokeza kipindi hiki.
“Dawasco
mbele kwa mbele”
Bi Everlasting Lyaro
Kaimu Meneja Uhusiano - Dawasco
0658-198889
Post a Comment