Header Ads

Watendaji Wanaotafuna Fedha za Miradi ya Wafadhili Mkoani Kigoma kukiona

Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Kigoma Bw. Daniel Machura akitoa hotuba ya kufunga mafunzo ya miradi ya maendeleo kwa ajili ya ufadhili wa washirika wa maendeleo kwa Mkoa wa kigoma. Kulia ni mmoja wa wakufunzi wa mafunzo hayo, Dkt. Wilhelm Ngasamiaku kutoka Chuo Kikuu  cha Dar es Salaam, kushoto ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Paul Sangawe kutoka Tume ya Mipango.

Mratibu wa Mafunzo Bw. Paul Sangawe akitoa muhtasari wa kile kilichojadiliwa katika mafunzo hayo yaliyodumu kwa muda wa siku tano. Katikati ni Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Kigoma Bw. Daniel Machura na kulia ni mmoja wa wakufunzi wa mafunzo hayo, Dkt Wilhelm Ngasamiaku kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mchumi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango - Tume ya Mipango, Bw. Senya Tuni akionesha kitabu cha Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/17-2020/21) kwa washiriki (hawapo pichani) wakati akiwasilisha mada juu ya Mpango huo.

Baadhi ya washiriki wakifanya mazoezi ya kanuni zinazotumika kuchagua miradi sahihi kwa ajili ya kupata ufadhili kutoka kwa washirika wa maendeleo. Mazoezi hayo yalifanyika mapema kabla ya kuhitimishwa kwa mafunzo hayo.

No comments

Powered by Blogger.