Header Ads

Jivu la mwili wa Fidel Castro lazikwa Santiago, Brazil

Jivu la aliyekuwa rais wa Cuba Fidel Castro limezikwa katika kiunga cha makaburi mjini Santiago, na hivyo kumaliza siku tisa za maombolezo ya kitaifa nchini Cuba.
Familia na wageni wachache walialikwa katika shughuli hiyo ya faragha, iliyofanywa karibu na makumbusho ya shujaa wa uhuru wa Cuba, Jose Marti.
Hapo jana, rais wa Cuba, Raul Castro, amesema serikali yake itakataza barabara au eneo lolote kupewa jina la Fidel, na ndivyo Fidel mwenyewe alivyoagiza.
Mbele ya mhadhara mkubwa mjini Santiago, alisema Fidel Castro hakutaka kufanywa kama kiongozi wa madhehebu.

No comments

Powered by Blogger.