Wadau wa Kilimo Kanda ya Ziwa Wapewa Somo Kuhusu Kilimo Bora
Katibu Tawala Msaidizi idara ya Uchumi na Uzalishaji mkoani Mwanza, Joanen Kukwami akifungua mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza kwa siku mbili, jana Novemba 03 na leo Novemba 04, 2016.
Mkutano huo uliandaliwa na Jukwaa la Wadau wa Kilimo nchini ANSAF, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kuhakikisha kunakuwa na kilimo chenye tija katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ili familia ziweze kujikimu kiuchumi na ki chakula.
Wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa wakimsikiliza Katibu Tawala Msaidizi idara ya Uchumi na Uzalishaji mkoani Mwanza, Joanen Kukwami wakati akifungua mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza kwa siku mbili, jana Novemba 03 na leo Novemba 04, 2016.
Meneja Mradi wa Jukwaa la Wadau wa Kilimo nchini ANSAF, Diana Lugano, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza kwa siku mbili, jana Novemba 03 na leo Novemba 04, 2016.
Wadau wa kilimo wakimsikiliza Meneja mradi wa ANSAF wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza.
Mratibu na Mchambuzi wa Sera na Bajeti kutoka Jukwaa la Wadau wa Kilimo nchini ANSAF, Joseph Nyamboha, akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza.
Mratibu na Mchambuzi wa Sera na Bajeti kutoka Jukwaa la Wadau wa Kilimo nchini ANSAF, Joseph Nyamboha, akiwasilisha mada kwenye mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza.
Jimmy Luhende ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Demokrasia na Utawala bora nchini, akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa Kilimo Kanda ya Ziwa.
.........................................
Upungufu wa
maafisa kilimo pamoja na uuzaji wa mbegu zisizo na ubora katika mikoa ya kanda
ya ziwa umeelezwa kusababishwa sekta ya kilimo katika mikoa hiyo kuzorota.
Hayo
yalibainishwa jana Jijini Mwanza kwenye mkutano wa wadau wa kilimo uliolenga kujadili
namna bora ya kuboresha sekta hiyo.
Walisema
baadhi ya maafisa kilimo waliopo katika mikoa ya kanda ya ziwa kushindwa
kuwafikia wakulima na kuwapatia elimu ya kilimo husababisha kilimo kisicho na
tisha huku uuzaji wa mbegu za kilimo zisizoota ukikwamisha kabisa juhudi za
wakulima kulima zao hilo.
Mkutano huo
uliandaliwa na Jukwaa la wadau wa kilimo nchini ANSAF na kuwakutanisha wadau
mbalimbali wa kilimo wakiwemo wakulima, viongozi wa serikali pamoja na taasisi
binafsi ambapo pamoja na mambo mengine umeadhimia kufikisha elimu kwa wakulima
ili kulima kilimo chenye tija.
Post a Comment