Mhandisi FELCHESMI MRAMBA akagua Vituo vya Kupooza na Kusambaza Umeme
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini, (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, (katikati), akizungumza wakati alipotembelea kituo kipya cha kupooza na kusambaza umeme cha City Centre jijini Dares Salaam, Novemba 5, 2016. Kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Miradi ya Usafirishaji na Usambazaji Umeme wa Shirika hilo, Mhandisi Gregory Chegere, na kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Shirika hilo kanda ya Dar es Salaam na Pwani Mhandisi, Mahende Mgaya.
Mhandisi Mramba, akizungumza na waandishi wa habari kwenye kituo cha Kupoozea na kusambaza umeme cha Ilala Mchikichini jijini Dar es Salaam |
Na KHALFAN SAID
MKURUGENZI
Mtendaji wa Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba,
ametembelea vituo vitatu vipya vya kupooza na kusambaza umeme vilivyo kwenye
mradi wa uboreshaji wa huduma za umeme jijini Dar es Salaam leo Novemba 5,
2016.
Vituo
alivyotembelea ni pamoja na kile cha katikati yajiji, (City Centre), kilicho
jirani na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Kituo cha Kurasini na kituo cha
Ilala Mchikichini.
Kwa
takriban mwezi mmoja sasa, TANESCO kwa kushirikiana na wahandisi kutoka kampuni
za Kijapani, Yachiyo Engineering Co Limited, Sumitomo, Takaoka na National
Construction Limited, wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kubadilisha laini kutoka
umeme mdogo kwenda umeme mkubwa, lakini pia kubadilisha vifaa vingine muhimu
ili kuwezesha usafirishaji umeme uweze kuwafikia watumiaji katika ubora wa hali
ya juu.
“Nimeridhishwa
na hatua iliyofikiwa ya kubadilisha miundombinu yetu ya umeme, wakazi wa jiji
la Dar es Salaam, sasa watapata umeme wa uhakika na ulio na ubora wa hali ya
juu, jambo la kufurahisha sana ni kwamba mabadiliko haya yamekwenda sambamba na
mipango ya Serikali ya awamu ya Tano ya kuifanya nchi yetu kuwa nchi ya viwanda,
bila shaka umeme huu utawezesha kufikia azma hiyo ya serikali.” Alisema
Mhandisi Mramba, baada ya kukagua kituo cha kupooza na kusambaza umeme cha
katikati ya jiji.
Mhandisi
Mramba alisema, nia ya TANESCO ni kuhakikisha wananchi wanaondokana na adha ya
kukatika umeme mara kwa mara au kupata umeme hafifu usio na nguvu. “Mmeona
mitambo hii nimipya kabisa nay a kisasa inayotumia teknolojia ya kisasa.”
Alitoa hakikisho.
Maboresgho
hayoyalihusisha ujenzi wa mfumo wa njia
ya usafirishaji umeme chini ya ardhi, (Underground Transmission Lines) , kutoka shule ya sekondari ya wasichana ya Jangwani
jijini Dar es Salaam na kutoka kituo cha umeme cha Makumbusho kwenda kituo
kipya cha kupoozea umeme kilichoko katikati ya jiji cha City Centre cha ukubwa
wa 100MVA (2X50MVA), 132/33KV, Kaimu Meneja wa Mradi huo, Mhandisi Iddi
Rashidi, alisema,
Alisema,
ujenzi wa mfumo huo wa njia ya umeme wa ardhini (Underground Distribution
Lines), wa kilomita 4.3 wa msongo wa kilovolti 33 ni kwa ajili ya kuunganisha
kituo cha City.
“Faida
kubwa ambayo wakazi wa jiji la Dar es Salaam watarajie ni kupata umeme wa
uhakika ulio kwenye viwango stahiki,
Naye Meneja Mwandamizi wa Miradi
yausafirishaji na usambazaji umeme wa Shirika hilo, Mhandisi Geirge Chegere,
alimueleza Mhandisi Mramba kuwa kituo cha City Centre cha 100MVA, kunafanya
jiji la Dar es Salaam pekee kuwa na jumla ya vituo 9 vya aina hiyo.
Mradi huo
unatarajiwa kuzinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuriya Muunganowa Tanzania, Dkt.
John Pombe Magufuli, baadaye mwezi huu wa Novemba.
Meneja Mwandamizi wa Usambazaji Umeme wa Shirika la
Umeme Tanzania, (TANESCO), ambaye pia ndiye Meneja wa Mradi wa kuimarisha
miundombinu ya Umeme, Injinia Theodory Bayona.akielezea hatuailiyofikiwa hadi sasa ya uboreshaji miundombinu ya umeme jijini Dar es Salaam.
Meneja Mwandamizi wa Miradi ya Usafirishaji na Usambazaji Umeme wa Shirika hilo, Mhandisi Gregory Chegere, akielezea teknolojia ya kisasa ya mashine ndogo yenye kufanya kazi kubwa.
Kituo cha City Centre.
Mhandisi Mramba, akitembelea mitamboya kituo cha City Centre.
Fundi mitambo ya umeme akiwa kazini kituo cha Ilala Mchikichini.
Mhandisi Mramba, (kushoto), akizungumza wakati alipotembelea kituo cha Kupooza na kusambaza umeme cha Kurasini kujionea maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho.
Mitambo ya kituo cha kupoozea na kusambaza umeme cha Kurasini.
Mhandisi Chegere (wapili kulia), akipatiwa maelezo ya mitambo ya kituo cha City Centre.
Jengojipya la kituo cha Ilala Mchikichini.
moja ya mashine mpya kituo cha Ilala Mchikichini.
Chumba cha mitambo mipya ya umeme kituo cha Ilala Mchikichini.
Mhandisi Mramba, akiwa na wahandisiwenzake, Chegere (kulia) na Mgaya, kwenye kituo cha City Centre.
Mitambomipya kituo cha Kurasini.
Post a Comment