Header Ads

Kampeni ya Binti wa Kitaa Wakazi wa Temeke Wapata Elimu Kuhusu Mimba na Ndoa za Utotoni

 Afisa Mtendaji wa Wilaya ya Tandika Hija Kipeleka akizindua Rasmi kampeni ya Binti wa kitaa katika Wilaya ya Temeke, ambapo aliwashukuru wanaoendesha kampeni hiyo na kuahidi kushirikiana nao katika kupinga mimba na ndoa za utotoni.

 Mkurugenzi Mtendaji wa CVIF George David  Maarufu kwa jina la Ambassador Angelo akielezea kwa kina kampeni ya Binti wa kitaa ilivyo wasaidia mabinti wengi na kutoa ufafanuzi wa kina juu ya kampeni hiyo ambapo kwa sasa inaendelea kuzinduliwa katika Wilaya zilizopo jijini Dar es Salaam.

 Mkazi wa Mtaa wa Mvomero Tandika Bi. Rauva Maulid akieleza namna akina baba walivyo na tabia ya kuwarubuni mabinti wenye chini ya umri wa miaka 18 na kuwababishia Mimba,na kuongeza kuwa kwa tandika watoto wengi wanapata mimba wakiwa na miaka kuanzia miaka 12.

 Mkazi wa Mtaa wa Mvomero Said Mgeni akisisitiza kuwa wazazi wanatakiwa kuwa jirani na watoto wao ili waweze kuwa rafiki na kuwaeleza matatizo wanayoyapata kwa sababu kwa kufanya hivyo mabinti watakuwa huru kueleza matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na tatizo la mimba.

 Aisha mkazi wa Tandika akieleza namna vijana wanavyowarubuni na kuwasumbua ili waweze kushiriki nao katika ngono uzembe.

 Wakiendelea kufuatilia kwa makini masomo mbalimbali wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Binti wa kitaa.

Picha na Fredy Njeje

No comments

Powered by Blogger.