Wasomi Waipongeza MeTL GROUP kwa Kufanya CAREERS FAIR
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya MeTL Group, Fatema Dewji-Jaffer akizungumzia idara yake ya masoko inavyofanya kazi wakati wa Kongamano la Ajira kwa Vijana waliomaliza vyuo ambao watapata fursa ya kupata ajira katika makampuni ya MeTL Group, lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Alliance Francaise.
Mtaalamu wa kilimo wa kampuni ya MeTL Group, Bw. George Mwamakula akizungumza wakati wa Kongamano la Ajira kwa Vijana waliomaliza vyuo ambao watapata fursa ya kupata ajira katika makampuni ya MeTL Group, lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Alliance Francaise.
Mtaalamu wa masuala ya fedha wa MeTL Group, Bi. Hasina Ahmed akizungumza wakati wa Kongamano la Ajira kwa Vijana waliomaliza vyuo ambao watapata fursa ya kupata ajira katika makampuni ya MeTL Group, lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Alliance Francaise.
Mtaalamu wa idara ya uzalishaji wa nyuzi na nguo ya MeTL Group, Bw. Clement Munisi akizungumza wakati wa Kongamano la Ajira kwa Vijana waliomaliza vyuo ambao watapata fursa ya kupata ajira katika makampuni ya MeTL Group, lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Alliance Francaise.
Na Mwandishi Wetu
Safari ya Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) kutoa ajira kwa Watanzania 100,000 hadi mwaka 2021 imeanza kufanyika kupitia Job Affairs ambapo limewapa nafasi wasomi mbalimbali nchini kutumia sehemu hiyo kuonyesha uwezo wao, na kati yao wasomi 25 wakipata nafasi ya kujiunga na familia ya zaidi ya wafanyakazi 28,000 wa kampuni ya MeTL Group.
Wakizungumza na waandishi wa habari baada ya kufanyika kwa kongamano hilo, wasomi mbalimbali waliipongeza kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited kwa kufanya kongamano la Job Affairs kwani licha ya kutoa nafasi za kazi lakini pia limewasaidia kujijengea uwezo mpya ambao hawakuwa nao awali.
Mmoja wa wasomi hao, Dennis Mtani alisema kupata nafasi ya kuhudhuria kumewajengea jambo lipya kuhusu jinsi ya kuomba nafasi za kazi hadi kuwa wafanyakazi bora katika kampuni.
Alisema kutokana na ukubwa wa kampuni ya Mohammed Enterprises kwa bara la Afrika ni matarajio yao kuwa wamejifunza jambo ambalo hata kama hawatapata nafasi za kazi basi watabaki na uwezo ambao utawasaidia kujua jinsi ya kuomba nafasi katika makampuni mengine ya kimataifa.
“Tumekuja katika kongamano hili wengine hata CV walikuwa hawajui jinsi ya kuandika ili kuomba nafasi na kuajiriwana na kutokana na ukubwa wa hii kampuni kwa nchi za Afrika tumepata elimu ambayo inaweza kutusaidia kwenda kufanya kazi kwa makampuni mengine,” alisema Mtani.
Nae Monica Mziray alisema alijumuika katika kongamano hilo ili kujaribu kutafuta nafasi ya kujiunga na kampuni ya Mohammed Enterprises kwani anaamini ni kampuni kubwa ambayo anaamini ana ndoto za kuifanyia kazi na ambayo inawajali wafanyakazi wake.
“Nimefanya kazi na kampuni zingine lakini niliacha sababu nataka kampuni ambayo inanilia vizuri na inanipa kitu na mimi naipa kitu, nilisoma historia ya Mohammed Enterprises, nimeona ni kampuni kubwa Afrika, nimeona bidhaa zake na naona inaweza niongezea kitu,” alisem Mziray.
Aidha akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo, Mkurugenzi wa Kitengo cha Rasilimali wa Mohammed Enterprises, Hassan Dewji aliwambia washiriki ambao wametoka katika taasisi mbalimbali za elimu ya juu, kwamba Idara ya Rasilimali Watu ya MeTL imekua ikitoa ajira, mafunzo ya kukuza vipaji kwa watanzania wa kada mbalimbali ili kuchukua nafasi za juu katika Makampuni shiriki ya MeTL.
Kuhusu kongamano hilo la kazi alisema linalengo la kupata wasomi wenye taaluma mbalimbali kutoka kwa vijana wa Kitanzania. Kwamba Idara ya Rasilimali Watu imelenga kupata wahitimu katika nyanja za Uhasibu wa fedha, Rasilimali watu, Masoko, Uhandisi, Kilimo na Viwanda vya nguo lakini pia vijana wasomi watapewa mafunzo kwa kipindi cha wiki 52 huku wakiwa wanalipwa na watakapomaliza mafunzo watapewa ajira na kuingizwa katika mfumo wa uwajibikaji.
“Kundi la Makampuni ya MeTL limepata umadhubuti wake kutokana na kuwa na utamaduni wa kuhakikisha kwamba wanakuwa karibu na wafanyakazi wake na kuwajali. Wafanyakazi wa Idara ya Rasimali Watu wamekua wakiandaa mafunzo kuboresha elimu ya wafanyakazi, maarifa na utaalamu,
“Ushiriki wa wafanyakazi ni sehemu ya maono ya wafanyakazi wa Idara ya Rasilimali Watu katika kundi hili la makampuni. Kampuni hii huhakikisha kwamba wafanyakazi wanapata mapumziko, kujitengeneza upya, wanakuwa na siku ya familia, siku ya michezo na kwamba shughuli hizo zinafanywa kwa mpangilio ili kuwezesha kuwepo kwa utamaduni wa familia moja inayofanya kazi kwa kushirikiana kwa kiwango cha juu,” alisema Dewji.
Post a Comment