Header Ads

Tanga UWASA yapata Tuzo ya Ubora kwa Mamlaka hapa Nchini

Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kushoto akipokea tuzo ya mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) ya ubora wa kimataifa,kupitia hati ya ISO 9001:2015 ulitokana na ushindi wa kuwa mamlaka bora ya hduuma za Maji Safi na Usafi wa Mazingira nchini kwa Mwaka 2014/2015 wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo,Salum Shamte.

 Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo,Salum Shamte kulia akipokea tuzo hiyo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella walioipata mamlaka hiyo ushindi wa kuwa mamlaka bora ya huduma za maji na usafi wa mazingira nchini mwaka 2014/2015.

  Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo,Salum Shamte kulia akimkabidhi tuzo hiyo Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa)Mhandisi Joshua Mgeyekwa anayeshuhudia katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella katikati akiwa na kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi ambapo kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi Mpya wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) Salum Shamte,Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira,Mhandisi Joshua Mgeyekwa wa kwanza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Abdulla Lutavi na Katibu Tawala Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi.
Mkuu wa Tanga,Martine Shigella akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa bodi mpya ya mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) uliyoteuliwa na Waziri wa Maji.
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) imeweza kuwa mamlaka ya kwanza nchini kufikia vigezo vya kupewa leseni ya EWURA ya Daraja la kwanza (Class 1Lesence).

Leseni hiyo ilitolewa Juni 17 mwaka huu na Waziri wa Maji na Umwagiliaji katika mkutano wa kuzindua ripoti ya mwaka 2014/2015 ya mamlaka za maji uliofanyika Mjini Dodoma.

Akizungumza mwishoni mwa wiki,Mkurugenzi Mkuu wa EWURA ,Felix Ngamlagosi  alisema kuwa leseni hiyo ilitolewa kwa Tanga Uwasa na kwa sasa ndio mamlaka ya maji pekee nchini iliyo na leseni ya EWURA ya daraja la kwanza nchini.

Alisema kuwa leseni hiyo ya daraja la kwanza imetolewa baada ya EWURA kupitia utendaji kazi wa Tanga Uwasa na kutadhimini viwango vilivyowekwa ili mamlaka ya maji kuweza kupata daraja la kwanza na kujiridhisha kuwa vimefikiwa.

Aidha alisema vigezo ambavyo vimeangaliwa kuwa mamkala bora ni kugharamia uendeshaji wa mamlaka,kugharamia uchakavu wa miundombinu na kuweza kulipia riba za mikopo ya uwekezaji.

  "Lakini pia uwezo wa Mamlaka hiyo kujitegemea kiufundi na kiuendeshaji"

Mkurugenzi huyo alisema kuwa mamlaka hiyo imeweza kuwa ya kwanza kwa miaka mitatu mfululizo miongoni mwa mamlaka kubwa 25 za maji zinazotoa huduma katika makao makuu ya mikoa Tanzania bara.

  Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa alisema wao kama mamlaka wataendelea kuhakikisha wanatoa huduma bora zinazoendena na viwango vikubwa ili kuendelea kuwa mamlaka bora nchini.

Alisema pamoja na changamoto walizokuwa nazo lakini wameweka mikakati kabambe ya kuhakikisha wanakabiliana nazo kwa kuwawezesha wananchi waweze kunufaika ana huduma ya Maji kwa kiwango kikubwa .


"Lakini pia sisi kama mamlaka tumejiwekea mipango kabambe ya kuhakikisha huduma za maji zinaimarika sambamba na kujiandaa na fursa ya ujio wa bomba la mafuta utakaoanzia nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga ili changamoto ya maji isiwepo wakati wa ujio wa fursa hiyo.

No comments

Powered by Blogger.