SONGAS Football Club Waendesha Bonanza la Kuhamasisha Michezo, Usafi na Afya Bora
Mechi mbalimbali zikiwa zinaendelea katika Bonanza hilo ambalo lilikuwa na lengo la kuhamasisha Michezo, usafi na Afya Bora.
Baadhi ya watu wadogo kwa wakubwa wakiendelea kufuatilia Bonanza hilo kwa makini.
MC Fadhili Nandonde akiendelea kutoa utaratibu wa Mechi mbalimbali zilizokuwa zikicheza katika Bonanza hilo.
Mgeni Rasmi katika Bonanza hilo Albert Kimaro ambaye ni Mkufunzi Mwandamizi Idara ya Michezo Chuo Kikuu cha Dar es salaam akikagua moja ya Timu hizo katika Bonanza hilo.
Mgeni Rasmi katika Bonanza hilo Albert Kimaro ambaye ni Mkufunzi Mwandamizi Idara ya Michezo Chuo Kikuu cha Dar es salaam akizungumza na watu waliofika katika bonanza hilo na kuwapongeza waandaaji kwa kuona umuhimu wa Mazoezi, usafi na Afya Bora pia amewasihi watu wawe na utaratiu wa kufanya Mazoezi.
Mwakilishi Kutoka Benki ya NMB ambao walikuwa ni moja ya wadhamini wa Bonanza hilo Frank Rwamugira akiwasihi watu kuwa na utaratibu wa kujiwekea akiba.
Watu mbalimbali wakiendelea kufuatilia Michezo hiyo , hata Boda boda nao walikuwa bize na Bonanza hilo.
Mbuzi huyu ndio ilikuwa zawadi ya Mshindi katika Bonanza hilo lililoandaliwa na Songas Football Club.
Post a Comment