Header Ads

TADB, PASS Wakubaliana Kusaidia Kilimo


Na Mwandishi Wetu,
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa kushirikiana na Mfuko wa Kusaidia Kilimo (PASS) wameingia makubaliano ya kudhamini mikopo kwa wakulima wasio na dhamana watakaokopa kupitia TADB.
Wakizungumza katika hafla ya kuwekeana saini makubaliano hayo, yaliyofanyika katika Ofisi za TADB, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Bw. Thomas Samkyi na Mkurugenzi Mkuu wa PASS, Bw. Nicomed Bohay wamesema kuwa katika kukabiliana na changamoto za ukosefu wa dhamana za uhakika, kunakochagiza ukosefu wa upatikanaji wa mikopo kwa wakulima taasisi hizo zimekubaliana kuwawekea dhamana wakulima wenye sifa ya kukopesheka katika Benki hiyo ila wanakosa dhamana waweze kudhaminiwa na PASS.
Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Bw. Francis Assenga (Kushoto) akizungumza wakati wa hafla ya kuwekeana saini makubaliano kudhamini mikopo kwa wakulima wanaokopa TADB. Kulia ni viongozi waandamizi wa TADB na PASS.
MkurugenziwaBiasharanaMikopowa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Robert Pascal (Katikati)akizungumza wakati wa hafla ya kuwekeana saini makubaliano kudhamini mikopo kwa wakulima wanaokopa TADB. Kulia ni viongozi waandamizi wa TADB na PASS. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti wa TADB, Bw. Francis Assenga (Kushoto) na Mkuu wa Sheria na Huduma wa Benki hiyo, Bibi Neema Christina John (Kulia). 
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi (Kushoto) akizungumza kabla ya kutiliana saini makubaliano yatakayowezesha wakulima wanaokopa TADB kupata dhamana kutoka PASS. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa PASS, Bw. Nicomed Bohay.
Wanahabari wakiwajibika wakati wa hafla ya kuwekeana saini makubaliano kudhamini mikopo kwa wakulima wanaokopa TADB.
Mkuu wa Sheria na Huduma wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB),, Bibi Neema Christina John (Kushoto) akigonga muhuri makubaliano yatakayowezesha wakulima wanaokopa TADB kupata dhamana kutoka PASS. Wanaoshuhudia niMkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi (Katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa PASS, Bw. Nicomed Bohay (Kulia). 
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi (Kushoto) akibadilishana hati za makubaliano yatakayowezesha wakulima wanaokopa TADB kupata dhamana kutoka PASS na Mkurugenzi Mkuu wa PASS, Bw. Nicomed Bohay (Kulia).
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi (Kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa PASS, Bw. Nicomed Bohay (Kulia) wakionesha hati za makubaliano yatakayowezesha wakulima wanaokopa TADB kupata dhamana kutoka PASS katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya TADB.

No comments

Powered by Blogger.