Header Ads

Jeshi la Polisi Lafungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi Jijini DAR ES SALAAM

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kushoto),  akipokelewa na Maofisa wa Jeshi la Polisi alipowasili Chuo cha Polisi Kilwa Road, kufungua Kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Jeshi hilo, jijni Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (katikati), akishiriki kuimba wimbo wa mshikamano kwa wafanyakazi wakati wa kufungua  mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa  Jeshi la Polisi uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Polisi, Kilwa road, jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Jeshi la Polisi wakishiriki kuimba wimbo wa mshikamano kwa wafanyakazi, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Baraza hilo uliofanyika Chuo cha Polisi Kilwa Road jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Jeshi la Polisi kilichofanyika Chuo cha Polisi, Kilwa Road jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Jeshi la Polisi wakiwa katika mkutano Baraza hilo  uliofanyika Chuo cha Polisi, Kilwa Road jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Abubakari Akida, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

No comments

Powered by Blogger.