Header Ads

TIGO Tanzania yadhamini Tamasha Kubwa la Muziki



Na Mwandishi Wetu, Iringa
 
Kampuni ya Tigo Tanzania imedhamini tamasha la muziki kwa wanamuziki chipukizi katika mikoa ya Kanda ya kusini ikiwa ni fursa ya wasanii hao  kuonesha vipaji vyao kwa wapenzi wa muziki. 
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kusini, Jackson Kiswaga, udhamini wa tamasha hilo liitwalo ‘Mtikisiko’ ni sehemu ya sera ya kampuni hiyo ya kusaidia makundi mbalimbali katka kijamii wakiwemo vijana na wasanii kufikia ndoto zao za kimaisha.

Akifafanua zaidi tamasha hilo Kiswaga, alisema bonanza la Mtikisiko litakuwa nyenzo ya kuwasaidia wanamuziki wapya kutoka mikoa ya Mbeya, Iringa, Njomba, Ruvuma na Rukwa kwa kuwatambulisha mbele ya mashabiki na wapenzi hivyo kuwaweka katika nafasi ya kujipatia kipato kutokana na kazi zao zao.

 “Udhamini huu umeonesha ni jinsi gani Tigo imedhamiria kusaidia kuendeleza mikakati na shughuli mbalimbali za ubunifu zinayofanywa na vijana katika harakati zao za kujiinua kiuchumi,” alisema Kiswaga.

Aidha Mkurugenzi huyo alisema mapema mwaka huu kampuni ya Tigo ilizindua huduma iitwayo Tigo Music ambayo inawapa wanamuziki nchini fursa ya kupakia nyimbo zao kwenye mtandao wao Internet na hivyo kuweza kusikilizwa na hadhira ya kitaifa na kimataifa jambo ambalo linawapa wasanii kipato cha ziada na fursa ya kujulikana kimataifa.

“Jukwaa la Tigo Music limetoa mchango  muhimu katika kuwanyanyua wasanii wanaoibukia  na kuchangia kuibuka kwa nyota wa ndani hadi kufikia viwango vya kimataifa. Ni matarajio yetu kwamba Bonanza hili la Mtikisiko ambalo litakalofanyika kwa kipindi cha wiki mbili litaibua majina na vipaji vipya katika Sanaa ya muziki nchini,” alisema Kiswaga
  

No comments

Powered by Blogger.