Header Ads

Mabondia HAMIS MWAKINYO na MESHACK MWANKEMWA kuzichapa Kesho

Bondia Hamisi Mwakinyo kushoto akitunishiana misuli na Meshach Mwankemwa baada ya kupima uzito leo kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa wa taifa unaotambuliwa na  Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania TPBC  katikati ni promomota kutoka katika kampuni ya Golden boy Afrika Shomari Kimbau.

Bondia Hamisi Mwakinyo kushoto akitunishiana misuli na Meshach Mwankemwa baada ya kupima uzito leo kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa wa taifa unaotambuliwa na  Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania TPBC utakaofanyika kesho katika ukumbi wa CCM Mwijuma Mwananyamala katikati ni promomota kutoka katika kampuni ya Golden boy Afrika Shomari Kimbau akiwa na mkanda utakaogombaniwa.

Mabondia Hamis Mwakinyo na Meshack Mwankemwa wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa wa KG 66 utakaofanyika katika ukumbi wa CCM Mwijuma mwananyamala Dar es salaam jumamosi.

Bondia Joyce Awino akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Asha Nzoa kushoto mpambano utakaofanyika kesho katika ukumbi wa CCM Mwijuma Dar es salaam kulia ni Rais wa kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBC Chaurembo Palasa.

Bondia Asha Nzowa kushoto akitunishiana misuli na Joyce Awino baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa kesho utakaofanyika katika ukumbi wa CCM Mwijuma Mwananyamala.

Promota Shomari Kimbau akiwainua mikono juu mabondia Asha Nzowa kushoto na Joyce Awino baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao kesho.

Rais wa Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBC Chaurembo Palasa akiwakumbusha baadhi ya sheria zitakazo tumika katika mchezo wa ngumi utakaofanyika kesho katika ukumbi wa CCM Mwijuma Mwananyamala Dar es salaam.

Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Meshack Mwankemwa na Hamisi Mwakinyo wamepima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa wa kg 66 unaotambuliwa na kamisheni ya ngumi za kulipwa nchi mkanda uho uliokuwa umeachwa wazi na bondia Selemani Zogo kwa kuto utetea kwa wakati sasa utapiganiwa na mabondia hawo kesho.

akizungumza wakati wa upimaji wa uzito promota wa mpambano uho Shomari Kimbau amesema mkanda uho utapiganiwa na mabondia hawo ili apatikane bingwa mpya wa uzito wa kg 66.

mpambano uho utasimamiwa na kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini chini ya rais wake Chauremba Palasa aliongeza kwa kusema mbali na mpambano uho siku hiyo pia kutakuwa na ngumi za utangulizi za mabondia mbalimbali.

Said Mayanga atamenyana na Gido Selemani wakati Mohamed Amir atapambana na Hemed Hemed.

na mpambano mwingine wa kusisimua utakuwa ni wa akina mama ambapo bondia mnaschachali Asha Nzowa 'Asha Ngedere' atapambana na Joyce Awino ambambao ambao unasubiliwa kwa hamu kubwa na mashabiki wanawake wa mchezo wa masumbwi.

No comments

Powered by Blogger.