Header Ads

Halmashauri Kuu ya CCM yapitisha Jina la Mgombea Ubunge LUDEWA

Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Halmashauri kuu ya CCM jijini Dar es salaam ambacho kimehudhuriwa kwa mara ya kwanza na Rais wa Awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli. 


 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM iliyofanyika leo tarehe 12 Novemba, 2015 chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete imemteua Ndugu Deogratius Ngalawa kuwa mgombea wake wa Ubunge katika Jimbo la Ludewa mkoani Njombe.

Ndugu Ngalawa ameteuliwa kugombea nafasi hiyo ya Ubunge baada ya kushinda kura za maoni zilizofanyika Novemba 10, 2015.

Imetolewa na:-


Daniel Godfrey Chongolo,    
Kny: KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI
12/11/2015




No comments

Powered by Blogger.