Header Ads

MWENYEKITI WA CUF PROF IBRAHIM LIPUMBA AZUNGUMZIA KUHUSU LOWASSA

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa IBRAHIM LIPUMBA akizungumza jambo na wandishi wa Habari (MAKTABA)
 
Na Mwandishi wetu 

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba ni kama amemshukia Edward Lowassa ambaye ni miongoni mwa Makada wa Chama cha Mapinduzi CCM ambao wanautaka urais kwa Udi na Uvumba kwa kusema ni Mtu hatari ambaye watanzania wanatakiwa kumwogopa.

Hayo yamesemwa na Profesa Lipumba leo Jijini Dar es Salaam Wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo Profesa lipumba amemtaka Mkurugenzi wa TAKUKURU Edward Hosea kumchunguza mara moja Edward Lowassa kwa hatua yake ya awali aliyotangaza nia kwa kusema ametumia pesa nyingi huku akionyesha wazi yeye ni mtumishi wa umma. 

 “Mimi nashangaa sana ofisi ya Hosea kuwa kimya kwa watu kama wakina Lowassa, ambao kutangaza nia tu wametumia gharama kubwa huko tunajua wazi hawa ni watumishi wa Umma wa siku nyingi pesa hizi wanazitoa wapi za kukodi mamia ya watu toka mikoa mbalimbali na kuwalipa posho kubwa.

Profesa Lipumba ameongeza kuwa kwa kusema hata Watangaza nia ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM kutumia pesa nyingi imeonyesha wazi kwamba walifanya makusudi “kunyofoa”Maoni ya Wananchi kwenye Katiba pendekezwa ambayo iliwabana watumishi wa Umma kutangaza mali zao zote. 

“Hawa wakina lowassa pamoja na wenzake walitumia nguvu kubwa kuzika maoni ya wananchi kwenye katiba ile husasani kwenye kipengele ambacho kinawataka Viongozi kutangaza mali zao pamoja na pesa wanazomiliki kabla ya kuwania sehemu mbali mbali za uongozi,kumbe walikuwa wanamalengo haya”ambainisha Profesa lipumba.

No comments

Powered by Blogger.