Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa mkandarasi
Nyanza Road Construction inayojenga barabara ya Furahisha hadi Pasiansi KM 2.8
wakati alipokagua ujenzi wa barabara hiyo, jijini Mwanza.
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemtaka Mkandarasi wa kampuni
ya Beijing Construction Engineering Group anayejenga uwanja wa ndege wa Mwanza kumaliza
kazi ya upanuzi wa uwanja huo ifikapo mwezi Februari Mwakani.
Profesa Mbarawa ametoa
kauli hiyo alipokuwa akikagua kazi ya ujenzi na upanuzi wa uwanja wa ndege wa
Mwanza pamoja na daraja la watembea kwa miguu lililopo maeneo ya furahisha,
jijini Mwanza.
Profesa Mbarawa
amesema kuwa kukamilika kwa ujenzi na upanuzi wa uwanja huo kutaimarisha hali
ya usafiri wa anga kwa wakazi wa Mwanza na mikoa mingine na hivyo kukuza
shughuli za kibiashara nchini.
“Hakikisheni upanuzi
wa uwanja wa ndege huu unakamilika haraka ili kurahisisha na kuboresha huduma
za usafirishaji kiwanjani hapa”, amesema Waziri Mbarawa.
|
Post a Comment