Mkurugenzi mteule wa Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga, ambaye ameteuliwa mwishoni
mwa wiki jana amesema anaamini ni Mungu aliyemuweka kwenye nafasi hiyo
ili awatumikie wananchi wa Mbulu kwa wakati huu.
Akiongea kwenye ibada
ya Jumapili hii ndani ya Kanisa la Living Water Center Kawe, wakati
alipopewa nafasi na mtumishi wa Mungu Apostle Onesmo Ndegi ili asalimia
Kanisa Mheshimiwa Kamonga alisema, anakwenda kwenye wilaya yenye
changamoto nyingi za kimaendeleo ila anaamini Mungu atamwezesha
kuzitatua kwa nafasi yake akishirikina na wananchi pamoja na viongozi
wengine kati halimashauri ya Mbulu.
Kamonga alisisitiza kuwa kwa kupata nafasi hii ya Ukurugenzi bado
ataendelea na utumishi wake kwa Mungu maana anaamini huo ndio uliomfanya
kufikia hatua hiyo,hivyo kuamua kuwa anamtanguliza Mungu kaika kila atakachokuwa anafanya,alisema Kamoga
Pia alitoa shukurani za dhati kwa Mtumishi wa Mungu Apostle Ndegi pamoja
na watumishi wengine kanisani hapo na kusema kuwa kati ya vitu ambavyo
hawezi kuvisahau na malezi mazuri ya kiroho pamoja na mafindisho ambayo
amekuwa akiyapata kutoka kwa Apostle Ndegi na watumishi wengine
kanisani hapo, akisema mafundisho hayo yamesababisha kuwa vile alivyo sasa!
Mwisho Mtumishi wa Mungu Mtume Onesmo Ndegi na waumini walifanya maombi
kwa ajili yake ili Mungu aambatane naye katika utumishi wake kwenye
nafasi hiyo ya Ukurugenzi!.
|
Mkurugenzi mteule wa Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga. |
|
Mkurugenzi mteule wa Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga akiwa na Baba yake wa Kiroho Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Center Kawe akimsiliza kwa makini akielezea uteuzi wake. |
|
Mkurugenzi mteule wa Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga akiwa na Baba yake wa Kiroho Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Center Kawe akimsiliza kwa makini akielezea uteuzi wake. |
|
Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Center Kawe akimwombea Hudson Kamoga akiwa amepiga magoti. |
|
Waumini wa Kanisani Living Water Center Kawe wakiwa wamenyoosha mikono kwa Hudson Kamoga kuomba kwa ajili yake |
Post a Comment